Image
Image

Uandikishwaji wapiga kura BVR Dar es Salaam waanza*Kitunda wasuasua.

BVR-Dar es Salaam.
Zoezi la uandikishaji wa wananchi katika daftari la kudumu la wapiga kura kwa njia ya kielektoniki – BVR limeanza leo jijini DSM
Waaandishi wa TAMBARARE HALISI wametembelea maeneo mbalimbali na kukuta wananchi wakiendelea na uandikishwaji katika daftari hilo la kudumu.
Baadhi ya maeneo ikiwemo kituo cha Sinza Lion mwandishi alikuta mashine ya kuandikishia wananchi ikiwa haifanyi kazi lakini baadae mashine hiyo ilitegenezwa na wataalamu kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi na zoezi kuendelea.
Waandikishaji wa vituo wamekuwa wakiwapa wananchi namba ili waweze kuandikishwa kiurahisi na kwakufuata foleni.

Zoezi hili la uandikishaji litadumu kwa muda wa wiki moja ambapo vituo vinafunguliwa saa 2 asubuhi na kufungwa saa 12 jioni.
MTAA WA IDRISSA MAGOMENI.
Issa Sekatawa Mwenyekiti Serikali za mtaa Iddrisa magomeni anasema kuwa Mtaa huu hali ni shwari na wananchi wanajitokeza kwa wingi katika suala zima la uandikishaji wapiga kura kwenye daftari la kudumu.
Nimefurahishwa na suala  moja katika uandikishaji watu wamepanga mistari kwa wake kwa waume kwa kuzingatia kuwa uandikishaji huo ni haki ya kila mtanzania aliyetimiza umri wa kupihga kura.
KATA YA KITUNDA.
Wilaya ya ilala kata ya kitunda inaelezwa uandikishaji huenda ukaleta mushkeli kwani hadi sasa mashine za kuandikisha bado zimekuwa kitendawili kufika ceneo hilo.
Wananchi wanasema waliopo ni mawakala wa vyama wakiwapa matumaini na kuwa wawe nasubira zitakuja na watajiandikisha kwa wakati.
Ingawa bado dalili za kuja kwa mashine hizo hawajajua bado.
Fuatilia Taarifa zetu tutakupa Update,Kila hatua inayokwenda.






Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment