Image
Image

Chipukizi wa Uswidi wabeba kombe la UEFA U19 barani Ulaya baada ya kuigaragaza Uhispania.


Timu ya taifa ya Uswidi ya kina dada wasiozidi umri wa miaka 19, walinyakuwa kombe la Ulaya baada ya kuicharaza Uhispania bao 3 – 1 kwenye fainali ya mashindano ya UEFA U19.

Magoli ya Uswidi yalifungwa na Stina Blackstenius katika dakika ya 28 na 36, pamoja na Filippa Angeldal katika dakika ya 89.

Uhispania nayo ilipata goli la kufutia machozi katika dakika ya 81 kupitia mchezaji Sandra Hernandez.

Ushindi huo umeiwezesha Uswidi kubeba kombe la UEFA U19 kwa mara ya tatu.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment