Image
Image

Breaking News:Ajali nyingine Basi la Sabuni Express Laua wanne baada ya kugongana na Land Cruiser Bugorora.



Watu wanne wanasadikiwa kufariki dunia baada ya Basi la Kampuni ya Sabuni Express linalofanya safari zake kati ya Karagwe na Mwanza kugongana uso kwa uso na Gari ndogo aina ya Toyota Land Cruiser iliyokuwa imebeba Masister eneo la Bugorora,ikitokea Bukoba mjini kuelekea Mutukura.

Ajali hiyo imetokea majira sambili asubuhi katika eneo la Bugorola wilayani Misenyi ambapo baadhi mashuhuda wa ajali hiyo wamesema ajali hiyo imetokea wakati Dereva wa gari ndogo aina ya landcruser alipokuwa akijaribu kulipita lori lililokuwa mbele yake na kisha kukutana uso kwa uso na basi la Sabuni Express lililokuwa na biria wapatao arobani na tano na kusabisha vifo vya watu wanne  ambao ni mapadri wawili,Sister mmoja na mseminalisti mmoja wote walikuwa wakisafiri na gari hiyo kuelekea karagwe.
Wakizungumza baadhi ya abiria waliokuwa wakisafiri na basi hilo wamsema dereva wa basi alikuwa katika mwendo wa kawaida kutokana ukungu ulikuwa kuwa umetenda barabarani.
Kwa upande wake katibu wa hospitali ya rufaa ya mkoa wa kagera Kiiza Kilwanila amesema wamepokea maiti nne pamoja na majeruhi kadhaa ambao sasa halizao zinaendelea vizuri.
TAMBARARE HALISI imefika katika kituo chapolisi mkoani Kagera kwaajili  kuthibitisha tukio hilo kwa kamanda wajeshi ambapo sikuweza kumkuta  na kujaribu kumtafuta kwa njia ya simu hakuweza kupatikana.

Kwa Taarifa zaidi Endelea kufuatilia Taarifa zetu kumbuka pia ku Like Page yetu hapo juu>>
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment