Waziri mkuu mstaafu Dokta.Salim
Ahmed Salim amesisitiza umuhimu wa kuimarishwa kwa misingi ya amani utulivu na
mshikamano wa kitaifa hasa kipindi hiki taifa likielekea katika uchaguzi mkuu
ambapo wanasiasa ndio wanajukumu kubwa la kuhakikisha wanasimamia misingi hiyo
ili nchi ya Tanzania iyendelee kuwa kisiwa cha amani na utulivu Duniani.
Dokta.Salimu ameyasema hayo
jijini Dar es salaam wakati akitoa
tathimini juu ya mustakabali wa hahali ya kisiasa ilivyo hivi sasa hapa
nmchini.
Amesema taifa sasa hivi limekosa
maadili ambapo yameporomoka kwa kiwango kikubwa tofauti na miaka ya nyuma jambo
ambalo linaogofya sana haswa katika nchi yetu hii inayo sifika kwa mambo mengi
mazuri.
“Maadili ya nchi hii yameporomoka
sana tu kwa kuwa mtu anataka uongozi si kwa sababu ya kutumikia wananchi bali
anataka uongozi wa jinsi gani ya kula nchi”amesema Dkt.Salm.
Dk.Salim amesema chama chochote cha siasa nchini kina nafasi ya kushika dola
endapo kitafuata kanuni na taratibu zilizowekwa na mamlaka husika,kwani
ikiangaliwa demokrasia katika vyama vya siasa imezidi kukua na kwamba kikubwa
kinachotakiwa ni kutumia njia bora na siyo kurushiana maneno ambayo
hayana msingi.“Utakuta viongozi wa vyama wenyewe kwa wenyewe wanarushiana maneno, huyu hafai mara siyo raia wa nchi hii, sasa haya mambo kwenye siasa hayatakiwi.
“Ni lazima kila kiongozi wa chama cha siasa atambue wajibu wake katika jamii,” alisema Dk Salim.
Amewaasa wananchi kuchagua viongozi bora kwa masilahi ya Taifa katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25 mwaka huu.
“Sasa kiongozi anagombea nafasi fulani kwa masilahi yake binafsi, siyo kwa wananchi na anawaomba wampigie kura,” alisema Dk Salim.
Aliwataka wananchi kuwa watulivu na kuilinda amani katika kipindi hiki cha uchaguzi.
Dokt.Salm anaongea hapa#Bofya hapo Kusikia,na kwa Taarifa Endelea kufuatilia Taarifa zetu kumbuka pia ku Like Page yetu hapo juu>>
0 comments:
Post a Comment