Hayo yamesemwa na mwanasheria wa NEMC Bw.Heche Suguta
wakati akizungumza jijini Dar es Salaama
ambapo amesema manispa ya ilala inapaswa
kuwaondoa wafanyabishara pale jangwani
kwa sababu eneo lile ni mkondo wa maji na hivyo hapapaswi kufanyiwa shughuli
zozote za kibinadamu.
TAMBARARE HALISI ilitembelea
katika eneo la jangwani ambapo
ilifanikiwa kuzungumza na wafanyabishara hao
ambapo walisema hawezi kuelewa agizo hilo kwani tayari wametumia fedha
nyingi kujenga na kuanzisha biashara hiyo
na hivyo wakiondoka pale nani atawalipa gharama walizotumia.
Naye kiongozi wawafanyabiashra
hao Bw.Denis David amehoji kama kweli
pale ni katika mkondo wa maji mbona kuna ujenzi mkubwa wa kituo cha mabasi cha
BRT natena mafuriko yalipotokea ulitokea
uharibifu mkubwa ila wao hawajaondolewa
na hivyo wameziomba mamlaka hizo za serikali kukaa na kutafakari tena.
Hata hivyo kituo hiki kilijaribu
kumtafuta mkurugenzi wa manispa ya ilala Isaya Mngulu bila ya mafanikio baada
ya kupiga simyu yake na yeye kujibu kuwa yupo katika mkutano wa kamati ya
ulinzi ya mkoa wakijadili zoezi la BVR na alipotafutwa afisa habari wa ilala
Bi.Tabu shaibu amesema hanataarifa kamili za kuwepo kwa barua hiyo labda
atafutwe mkugenzi.
0 comments:
Post a Comment