Image
Image

Familia za abiria waliofariki kwenye ajali ya ndege ya Germanwings zakana fidia ya fedha Euro 25,000.


Shirika la ndege la Lufthansa limeripotiwa kuwasilisha ombi la kutaka kutoa fidia ya fedha Euro 25,000 kwa kila abiria aliyepoteza maisha katika ajali ya ndege ya Germanwings iliyotokea Ufaransa.
Familia za abiria hao waliopoteza maisha zimekana kupokea fedha hizo kwa kudai kwamba ni kiasi kidogo mno kisichoweza kuwatosheleza.
Wakili wa familia za abiria Elmar Giemulla, aliandika barua kwa shirika la Lufthansa na kudhihirisha kupinga fidia hiyo ndogo ya fedha Euro 25,000.
Katika maelezo yake aliyotoa kwenye barua hiyo, Giemulla alisema, ‘‘Tunakana fidia hiyo kwa sababu haiwezi kuwatosheleza jamaa wa abiria waliofariki. Lufthansa inapaswa kutoa fidia ya fedha zisizopungua Euro 100,000 kwa kila familia.’’
Ndege ya Germanwings aina ya Airbus A320 ilianguka tarehe 24 mwezi Machi kusini mwa Ufaransa wakati ilipokuwa ikisafiri kutoka Barcelona kuelekea Düsseldorf. Wafanyakazi 6 wa ndege pamoja na abiria 144 walipoteza maisha kwenye ajali hiyo.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment