Hadi
jana, ambayo ilikuwa ni siku ya mwisho kwa vyama hivyo kuchukua na
kurejesha fomu, jambo moja lilijidhihirisha katika baadhi ya majimbo kwa
upande wa CCM; baadhi ya majina makubwa katika siasa za ubunge
yanachuana hivyo kufanya mchakato wa kumpata mteule mmoja kuwa mgumu.
Mchuano
huo na kuimarika kwa Chadema mikoani hasa kutokana na majeraha ya
mchakato wa urais ndani ya CCM, vinaufanya upinzani wa kuwania ubunge
katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu kuwa sawa na vita.
Nzega Vijijini
Makada wawili wa chama hicho, Lucas Selelii na Dk Hamisi Kigwangalla wamechukua fomu kuwania ubunge wa Nzega Vijijini.
Katika
uchaguzi uliopita wa 2010, makada hao walivaana katika Jimbo la Nzega
lakini wote wakaangushwa na Hussein Bashe aliyeibuka wa kwanza
akifuatiwa na Selelii.
Hata hivyo, matokeo hayo yalibatilishwa na Halmashauri Kuu ya CCM na kumchukua Dk Kigwangalla aliyekuwa mshindi wa tatu.
Mgawanyo
wa majimbo uliofanywa wiki iliyopita na Tume ya Taifa ya Uchaguzi
(NEC), umerahisisha mpambano wa makada hao, hivyo wawili hao wakamwachia
Bashe Nzega Mjini.
Akichukua fomu hiyo jana, katika
ofisi za CCM za Wilaya ya Nzega, Dk Kigwangalla akiwa ameambatana na
wazee wa jimbo hilo, alisema shinikizo la kugombea Nzega Vijijini
limetoka kwa wananchi wanaotambua umuhimu wake.
Selelii aliyekuwa Mbunge wa Nzega kwa miaka 15 hadi 2010, alichukua fomu kimyakimya bila kuzungumza na vyombo vya habari.
Katibu
wa CCM Wilaya ya Nzega, Empimark Makuya alithibitisha kuwa kada huyo
alishachukua fomu. Wawili hao watakabiliana na upinzani mkali kutoka kwa
wengine wawili waliochukua fomu, John Dotto na Paul Kabelele.
Maiga aibukia Iringa
Baada
ya kukwama katika harakati za kuwania urais kupitia CCM, Balozi Dk
Augustine Mahiga amejitokeza kuwania ubunge katika Jimbo la Iringa
Mjini.
Dk Mahiga aliyechukua fomu jana na kurudisha,
atapambana na Mwenyekiti wa CCM mkoani humo, Jesca Msambatavangu, Mkuu
wa Wilaya ya Wanging’ombe, Frederick Mwakalebela na mwandishi wa habari,
Frank Kibiki ambao tayari wamechukua na kurejesha fomu zao.
Mchuano
katika jimbo hilo unatarajiwa kuwa mkali wakati na baada ya kura za
maoni ndani ya CCM hasa ikizingatiwa kwamba Mwakalebela alikuwa
amechukua namba moja katika kura za maoni za chama hicho mwaka 2010
kabla ya jina lake kukatwa na NEC.
Mshindi atakuwa na
wakati mgumu kukabiliana na kishindo cha upinzani hasa kutoka Chadema
ambako Mchungaji Peter Msigwa aliyeshinda katika uchaguzi uliopita, jana
alipokewa na umati mkubwa wa watu alipowasili mjini hapo.
Profesa Maghembe na Thadayo tena
Mshikemshike
mwingine unatarajiwa kuibuka katika Jimbo la Mwanga ambako Waziri wa
Maji, Profesa Jumanne Maghembe anatarajiwa kupambana tena na hasimu wake
mkubwa katika kiti hicho, Joseph Thadayo.
Katika
uchaguzi wa 2010, Profesa Maghembe alimshinda Wakili huyo ambaye
alionekana kuungwa mkono na wanasiasa wengine wenye nguvu katika jimbo
hilo. Mbali yao wengine waliojitokeza ni Aminieli Kibali na Karia
Magaro.
Wasira, Bulaya wavaana
Mchuano
mwingine mkali unatarajiwa kuwapo katika Jimbo la Bunda Mjini ambako
Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Stephen Wasira atavaana na Mbunge
wa Viti Maalumu, Ester Bulaya.
Wabunge hao wa CCM
wamekuwa wakitambiana muda mrefu na wakati mwingine waliwahi kurushiana
maneno hadi bungeni, lakini mwisho wa tambo zote ni kwenye kura za
maoni.
Mamia warejesha fomu
Hadi
muda wa mwisho wa kurejesha fomu unakamilika saa 10 jioni jana, mamia
ya makada wa Chadema na CCM walikuwa wamejitokeza na kudhihirisha kuwa
mchuano utakuwa mkali katika kura za maoni na hata kwenye uchaguzi
wenyewe.
Kawe 22: Elias Nawera, Dk
Walter Nnko, Jumaa Muhina, Kippi Warioba, Atulinda Barongo, Tegemeo
Sambili, Kiganga George, Edmund Lyatuu, Charles Makongoro Nyerere, Mtiti
Butiku, Yusuf Nassoro, John Mayanga, Dickson Muze, Dk Wilson
Babyebonela, Colman Massawe, Amon Mpanji, Amelchiory Kulwizira, Gabriel
Mnasa, Abdallah Majura na Jerry Murro, wote wakikabiliana na Halima Mdee
aliyejitokeza pekee Chadema, hasa iwapo atasimama pekee kupitia Ukawa.
Kinondoni 12:
Idd Azan, Wagota Salum, Tonny Kalijuna, Goodchange Msangi, Emmanuel
Makene, Lusajo Willy, Mage Kimambi, Mussa Mwambujule, Stevew Nengere
(Steve Nyerere), Joseph Muhonda, Michael Wambura na Macdonald Lunyiliga.
Ubungo 12:
Vincent Mabiki, Timoth Machibya, Jordan Baringo, Emmanuel Mboma,
Zangina Zangina, Kalist Ngalo, Hawa Ng’umbi, Jackson Millengo, Didas
Masaburi, Joseph Massana, wote wa CCM wakitarajiwa kumkabili John Mnyika
wa Chadema.
Ilala watatu: Mussa Azzan Zungu, Mrisho Gambo na Waziri Kindamba.
Ukonga 16:
Jerry Silaa, Jacob Katama, Hamza Mshindo, Frederick Rwegasira, Anthony
Kalokola, Ramesh Patel, Peter Majura, Amina Mkono, Edwin Moses, Robert
Masegese, John Bachuta, Edward Rabson, Nickson Tugale, Elly Ballas, Asia
Msangi, Lucas Otieno, Fredrick Kabati, Mwanaidi Maghohe, Mwita Waitara,
Deogratius Munishi, Deogratius Kalinga, Deogratius Mramba, Salanga
Kimbaga, James Nyakisagana, Lameck Kiyenze na Gaston Makweta.
Segerea 13:
Zahoro Lyasuka, Apruna Humba, Bona Kalua, Nicholaus Haule, Baraka
Omary, Benedict Kataluga, Dk Makongoro Mahanga na Joseph Kessy.
Kigamboni 10:
Aron Othman, Kiaga Kiboko, Abdallah Mwinyi, Dk Faustine Ndugulile,
Ndahaye Mafu, Flora Yongolo, David Sheba, Mohammed Ally Mchekwa, Khatib
Zombe na Adili Sunday.
Mbagala 23:
Lucas Malegeli, Mindi Kuchilungulo, Kazimbaya Makwega, Adadius Richard,
Tambwe Hiza, Issa Mangungu, Ingawaje Kajumba, Siega Kiboko, Peter
Nyalali, Mwinchumu Msomi, Dominic Haule, Aman Mulika, Banda Sonoko, John
Kibasso, Ally Makwiro, Alvaro Kigongo, Maesh Bolisha, Kivuma Msangi,
Deus Sere, Abdulrahim Abbas, Salum Seif Rupia, Ally Mhando, Fares
Magessa, Stuwart Matola.
Moshi:
Priscus Tarimo, Amani Ngowi, Patrick Boisafi, Davis Mosha, Buni Ramole,
Halifa Kiwango, Michael Mwita, Daud Mrindoko, Shanel Ngunda, Innocent
Siriwa, Edmund Rutaraka, Omari Mwariko, Basil Lema, Jaffar Michael na
Wakili Elikunda Kipoko.
Busokelo:
Suma Mwakasitu , Dk Stephen Mwakajumilo, Ezekiel Gwatengile, Mwalimu
Juma Kaponda, Ally Mwakibolwa, Issa Mwakasendo, Aden Mwakyonde na
Lusubilo Mwakibibi.
Kilombero: Kanali
mstaafu Harun Kondo, Vitus Lipagila, Abdullah Lyana, Oscar Mazengo,
Japhet Mswaki, Paul Mfungahema, John Guninita, Abubakari Asenga na Abdul
Mteketa.
Mlimba: Dk Frederick
Sagamiko, Senorina Kateule, Godwin Kunambi, Augustino Kusalika, George
Swevetta, Castor Ligallama, Profesa Jumanne Mhoma, Fred Mwasakilale,
Dismas Lyassa.
Namtumbo: Edwin
Ngonyani, Edwin Milinga, Mwinyiheri Ndimbo, Vita Kawawa, Anselio
Nchimbi, Julius Lwena, Fitan Kilowoko, Balozi Salome Sijaona, Mussa
Chowo, Salum Omera, Ally Mbawala na Charles Fussi.
Tunduru Kaskazini:
Mhandisi Ramo Makani, Omary Kalolo, Michael Matomola, Hassan Kungu,
Issa Mpua, Rashid Mandoa, Athuman Mkinde, Shaban Mlono na Moses
Kulawayo.
Tunduru Kusini: Abdallah Mtutura, Daim Mpakate na Mtamila Achukuo.
Nyasa:
Christopher Chale, Bethard Haule, Adolph Kumburu, Alex Shauri, Frank
Mvunjapori, Dk Steven Maluka, Stella Manyanya, Cassian Njowoka, Jarome
Betty na Oddo Mwisho.
Serengeti: Dk Stephen Kebwe, Dk James Wanyancha, Juma Kobecha na Mabenga Magonera.
Sumbawanga Mjini:
Aeshi Hilaly, Anyosisye Kiluswa, Fortunata Fwema, Mathias Koni, Gilbert
Simya, Frank Mwalembe, Selis Ndasi, Mbona Mpaye, Sospeter Kansapa,
Paschal Sanga na Victor Vitus.
Korogwe Vijijini:
Stephen Ngonyani (Profesa Majimarefu), Cesilia Korassa, Allan Bendera,
Ali Mussa Moza, Abdallah Nyangasa, Christopher Shekiondo, Andrew Matili,
Edmund Mndolwa, Ernest Kimaya, Peter Mfumya na Stephen Shetuhi.
Kilindi: Beatrice Shellukindo, Abdallah Kidunda, Fikirini Masokola na Dk Aisha Kigoda.
Bariadi Mashariki: Masanja Kadogosa na Joram Masaga.
Mbulu: Mary Margwe amechukua fomu ya kugombea ubunge wa viti maalumu
Mbunge wa Arumeru Magharibi, Goodluck Ole Medeye na yule wa Kilosa Kati, Mustafa Mkulo hawakujitokeza kuchukua fomu.
Imeandikwa
na Julius Mathias, Bakari Kiango, Godfrey Kahango, Ngollo John, Salim
Mohammed, Joseph Lyimo, Faustine Fabian, Joyce Joliga, Daniel Mjema,
Burhani Yakub, Antony Mayunga, Mussa Mwangoka na Mustapha Kapalata
0 comments:
Post a Comment