Fenesi ni miongoni mwa matunda ya msimu yenye umbo la kipekee na
ladha tamu ya aina yake.
Tunda hili linatajwa kuwa na faida
lukuki kiafya kwa mwili wa mwanadamu.
Kula gramu 100 tu ya fenesi huweza
kuupatia mwili nguvu ya kalori 95, na tunda hili lina nyama laini
iliyojaa sukari aina ya fructose na sacrose inayoweza kuupatia mwili
nguvu na kuuhuisha kwa haraka.
Fenesi limejaa ufumweli au fibre, sifa
inayosaidia kulainisha choo,Tunda hili lina virutubisho kadha wa kadha
vyenye faida kubwa mwilini. Baadhi ya virutubisho hivyo ni vitamini A,
C, B complex, vitamin B6, folic acid, niacin, riboflavin na madini za
aina mbalimbali kama vile potassium, magenesium, manganese na chuma,Katika tunda la fenesi kuna protini, mafuta, wanga na antioxidants.
Fenesi pia linatajwa kuwa chanzo kizuri cha nishati kisichokuwa na
mafuta,Si hayo tu,bali pia kwa kuwa na virutubisho vyenye uwezo wa
kuondosha sumu mwilini,tunda hilo linaweza kuukinga mwili dhidi ya
saratani na magonjwa mengine na pia kuongeza uwezo wa kuona.
Kiasi
kikubwa cha madini ya potassium kinachopatikana katika fenesi hulifanya
tunda hili liwe na uwezo pia wa kuimarisha mifupa na afya ya ngozi.
Wataalamu wa afya wanasema fenesi huongeza ufanisi wa mfumo wa kinga
mwilini na kusaidia kuongeza kinga dhidi ya kifua,mafua na kikohozi.
Hii ni kwa sababu ya kuwa na vitamini za aina mbalimbali,Faida nyingine
ni kurekebisha msukumo wa damu na pia husaidia kurahisisha mmeng'enyo
wa chakula tumboni pamoja na kuukinga mwili dhidi ya magonjwa ya moyo na
kupooza.
Sio vibaya kuelewa kuwa inasadikika kwamba tunda hili lina
uwezo wa kuukinga mwili dhidi ya ugonjwa wa pumu na kupunguza makali ya
ugonjwa huo.
Si hivyo tu,bali fenesi lina vitamini muhimu
zinazohitajika kwa ajili ya utengenezaji wa damu mwilini.
Home
Afya
Fenesi husaidia kurekebisha msukumo wa damu na pia kurahisisha mmeng'enyo wa chakula tumboni.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment