Hamad, Mbunge wa Wawi (Cuf) anayemaliza muda wake na sasa
amejiunga na ADC, aliyasema hayo wakati chama hicho kikikabidhi fomu kwa
wagombea wa nafasi ya urais wa Jamhuri ya Muungano kupitia chama hicho.
Alisema katika kipindi hiki ambacho uandikishaji unafanyika sehemu
mbalimbali nchini kupitia mfumo wa Biometric Voters Registration (BVR),
kumebainika changamoto mbalimbali ambazo zinaashiria baadhi ya wananchi
kushindwa kupata haki ya kujiandikisha.
Hamad alisema ni vema Nec ikafanya haraka kutatua changamoto hizo ili kutoa fursa kwa wananchi wote kujiandikisha.
Alisema hata katika maeneo ambayo kazi hiyo imekwisha malizika,
lakini kuna watu ambao hawakuandikishwa, ni vema ikahakikisha nao pia
wameandikishwa.
"Kazi ya uandikishaji katika daftari la wapigakura ni muhimu kwa
mustakabali wa taifa, lakini mwaka huu imegubikwa na changamoto nyingi,
idadi ya watu wanaohitajika kuandikishwa ni wengi na vifaa vilivyopo ni
vichache," alisema na kuongeza:
"Ni rai yangu kwa Tume ihakikishe inatatua haraka changamoto
zinazojitokeza katika shughuli hiyo ili raia wote wa Tanzania
wanaostahili wajiandikishe kwa kuwa ni haki yao Kikatiba."
Kadhalika, Hamad aliitaka Nec kusimamia na kutokwenda kinyume cha
sheria za uchaguzi katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu.
Alisema Nec pekee ndiyo itasaidia uchaguzi huo uwe huru na wa amani
endapo itasimamia sheria za uchaguzi ikiwamo kuepuka kuweka upendeleo
kwa chama chochote cha siasa.
"Ninaiomba Tume katika uchaguzi huu, iepuke sana kupindisha sheria
za uchaguzi kwa kupendelea chama chochote, inatakiwa kutenda haki kwa
vyama vyote bila kujali ukubwa wake wala udogo wake na hiyo ndiyo njia
pekee itakayosaidia uchaguzi huo ufanyike katika hali ya amani na
utulivu.
Pia aliwaasa viongozi wanaowania nafasi mbalimbali za uongozi mwaka
huu, kuwasikiliza wananchi wa hali ya chini kwa kuhakikisha wanapatiwa
haki zao za msingi.
0 comments:
Post a Comment