Madaktari wanaohudumu katika hospitali za umma nchini Ghana, wametangaza kuchukuwa hatua ya kufanya mgomo kote nchini kwa lengo la kudai uboreshaji wa huduma za kazi.
Madaktari hao pia walitishia kujiuzulu endapo serikali itashindwa kuleta utatuzi kuhusiana na ombi lao ndani ya wiki moja.
Shirika la madaktari la Ghana (GMA), liliarifu kwamba madaktari wataanza kusitisha huduma za matibabu kwenye kitengo cha OPD kwa muda wa wiki moja ili kushinikiza serikali.
Kwa mujibu wa GMA, madaktari wamekuwa wakiwajibika kwa nchini Ghana kwa miaka mingi bila ya stakabadhi yoyote inayobainisha hali ya huduma za kazi.
Baadaye GMA ikafanya makubaliano na serikali ya Ghana ili kufanya maboresho hadi ifikiapo tarehe 28 mwezi Juni ingawa tarehe hiyo ilibadilishwa na kuwa Julai 28.
Licha ya wizara ya kazi kutangaza maafikiano na GMA kuhusiana na utatuzi wa mzozo huo, madaktari wameonaka kushikilia msimamo wao wa kufanya mgomo wa kitaifa nchini Ghana.
0 comments:
Post a Comment