Dk
Magufuli akitokea Mwanza, alivuka Ziwa Victoria na kuingia Sengerema
huku wavuvi waliokuwa wakitumia mitumbwi wakipeperusha bendera za CCM na
kukizunguka kivuko cha Mv Misungwi alichokuwa ameabiri pamoja na
msafara wake.
Msafara wa Dk Magufuli ulioanzia kwenye
Kivuko cha Busisi saa 3.35 asubuhi ulisimamishwa mara kadhaa na wananchi
ambao walikuwa wamefunga barabara wakiwa na matawi ya miti na wengine
wakitembea kuusindikiza.
Dk Magufuli ambaye alikuwa
ameambatana na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nauye na Naibu
Katibu Mkuu wa CCM Tanzania Bara, Rajabu Luhwavi alikuwa akisimama
kwenye gari la wazi na kuwapungia wananchi waliyokuwa wamejipanga kwenye
Barabara Kuu ya Geita- Bukoba.
Mapokezi ya Dk Magufuli
yaliongozwa na Mbunge wa Sengerema, William Ngeleja ambaye gari lake
ndilo lililokuwa limetangulia huku likisimama kwenye makundi ya watu na
kuwapanga kutokana na wingi wao. Msafara huo pia uliongozwa na ving’ora
vya polisi, huku ukiwa umetawaliwa na magari ya wabunge wa CCM kutoka
mikoa mbalimbali ya Kanda ya Ziwa.
Geita yarindima
Msafara
wa Dk Magufuli ulifika mkoani Geita saa 5.30 asubuhi na barabara
zilifungwa kwa dakika 15 wakati mgombea huyo akisalimiana na wakazi wa
mkoa huo.
Akizungumza wakati akisalimiana na wakazi wa
Sengerema na Geita, Dk Magufuli alisema amepita kuwasalimu na huku
akiwaahidi kuwa hatawaangusha...
“Nimekuja kuwasalimia,
itoshe kusema kwamba sitawaangusha. Nimefundisha shule ya Sekondari
Sengerema hivyo hapa ni nyumbani,” alisema Dk Magufuli.
Awali,
Dk Magufuli alianza kwa kuimba wimbo wa Kisukuma, “aliselema” huku
wananchi wakiitikia ‘alija’ “aliselema”, ‘alija’ “selema, selema, aleja,
ng’wana ngosha, ‘aleja.’ Wimbo huo unamaanisha “anasukuma, anakwenda,
mtoto wa kiume, anakwenda.”
Baada ya kuimba wimbo huo,
Dk Magufuli alianza kwa kuwashukuru wananchi wa Geita kwa mapokezi
makubwa ambayo hayajawahi kutokea tangu awe kiongozi... “Wana Geita
nawashukuruni sana kwa mapokezi haya... yanaonyesha ni mapokezi ya
ushindi, nimebaki na deni kubwa kwenu, nitawatumikia wananchi wote na
sitawaangusha, sitajali chama nitawatumikia wote wa CUF, UDP, Chadema,
CCM sitajali huyu ni wa chama gani, nashukuru sana wananchi wa Geita,”
alisema na kuongeza: “Leo si siku ya kampeni, nikianza watasema nimeanza
kampeni mapema. Mimi napenda kusema kwamba wanashukuru sana wana Geita
kwa sala zenu zilizonifikisha hapa leo, nitafanya kazi kwa ajili ya
Watanzania wote, sitawabagua.
0 comments:
Post a Comment