Taarifa ya kushikiliwa kwa wahalifu hao sita na jeshi la polisi imewekwa wazi na kamanda wa polisi kanda maalum Dar es Salaam Suleiman Kova mbele ya waandishi wa habari ikiwa ni muendelezo wa kuwasaka wote waliohusika na uvamizi wa kituo na kufanya mauaji.
Katika tukio hilo wahalifu hao walipora bunduki zinazodaiwa
kufikia 20 na pia shehena ya risasi waliyoihifadhi kwenye gunia.
Dar es Salaam.
Dar es Salaam.
Kwamujibu wa kamanda KOVA kwa ushirikiano
mzuri na wananchi wamefanikiwa kukamata bunduki 16 na14 zikiwa ni zile
zilizoibiwa katika tukio la kituo cha Stakishari na mbili zikiwa bado
hazijulikani wapi zimeporwa.
Taarifa njema kwa wananchi ambazo
zililifikia Jeshi hilo la polisi zilidai kuwa silaha zilizoibiwa kituo cha
stakishari zimehifadhiwa mkuranga jambo ambalo likafanya jeshi hilo kupiga
kambi ili kuweza kunasa wafichaji wa silaha hizo pamoja na kuwa kamata.
Kova amesema eneo la Twangoma huko
mbagala kwa umakini mkubwa na mzito jeshi hilo lilijipanga vyema na hivyo
kuweza kufika walipo majambazi hao na kukabiliana nao ambapo walifanikiwa
kuwatia nguvuni majambazi watano lakini katika kuendelea kukabiliana nao watatu
walifariki na wawili wanao wakiwa hai bado.
Amesema silaha hizo zilikuwa
zimefichwa kwenye eneo ambalo kulionekana nisehemu ambayo kulikuwa
kumeehifadhiwa kinyesi cha bina damu ndipo jeshi hilo lilipokuwa na shaka napo
hivyo kuchimba na hivyo kufanikiwa kupata silaha hizo,Bunduku 16 kumi na 14 zikielezwa ziliporwa kituo cha stakishari,Risasi
55 huku risasi 28 ni zile zilizoibiwa katika tukio la stakishari.
Licha ya kukuta silaha na risasasi
katika upande mwingine lilikuta Sanduku lililokuwa fedha kiasi cha shilingi
million sabini ambazo hazikujulikana mara moja zilikuwa na lengo gani.
Kova amesema kuwa pamoja na mafanikio
hayo yaliyopatikana katika operation hiyo bado jeshi la polisi kanda maalum ya
Dar es salaam linaendelea na kazi kubwa ya kuwasaka wahalifu hao kwa kuwa bado
kuna silaha nyingi ambazo ziliporwa katika kituo cha polisi Stakishari Ukonga
Dar es Salaam.
Endelea kutembelea mtandao wetu kupata taarifa.
0 comments:
Post a Comment