Jengo la chama cha AKP mjini Izmir lashambuliwa kwa grunedi.
Shambulio la kigaidi katika jengo la AKP mjini Izmir limeharibu jengo hilo pamoja na gari iliyokuwa imeegezwa mbele ya jengo hilo. Hakuna aliyejeruhiwa katika shambulio hilo.
Hatua zaidi za usalama zimechukuliwa ili kuimarisha usalama katika eneo hilo.
Akikashifu shambulio hilo mbunge wa Izmir Kerem Ali Surekli alisema, "Hatutakubali amani itishiwe nchini humu."
Mkuu wa chama cha AKP katika eneo la Izmir Bulent Delican alisema kuwa shambulio hilo lililenga uhuru na umoja nchini humo.
0 comments:
Post a Comment