Joe Jackson afikishwa hospitalini baada ya kushikwa na kiharusi cha ghafla nchini Brazil.
Mzee Joe Jackson ambaye ni babake marehemu Michael Jackson, ameripotiwa kufikishwa hospitalini mjini Sao Paulo baada ya kukumbwa na ugonjwa wa kiharusi nchini Brazil.
Joe Jackson alikuwa amesafiri Sao Paulo nchini Brazil kwa ajili ya maandalizi ya sherehe ya siku ya kuzaliwa ya mwaka wake wa 87 iliyotarajiwa kufanyika kwenye kilabu moja ya kifahari ya golfu.
Baadaye Joe Jackson akalazimika kufikishwa katika hospitali ya Albert Einstein baada ya kushikwa na ugonjwa wa kiharusi.
Kwa mujibu wa maelezo yaliyotolewa hospitalini, Joe Jackson aliwekwa kwenye kitengo maalum cha matibabu kutokana na kushikwa na ugonjwa wa kiharusi katika iskemia unaohusishwa na mapigo ya moyo yasiyokuwa ya kawaida.
Hapo awali, Joe Jackson pia aliwahi kushikwa na ugonjwa wa kiharusi mara tatu, mwisho ikiwa ni mwaka 2012 mjini Las Vegas.
Ingawa Joe Jackson mwenyewe ambaye ni mhusika mkuu alikosekana, sherehe yake ya kuzaliwa iliendelea kama ilivyopangwa na wageni 180 waliohudhuria.
0 comments:
Post a Comment