Jaji wa Mahakama ya Rufaa Tanzania, Mbarouk Salum Mbarouk amesema katika uchaguzi Mkuu uliopita mwaka jana kulikua na pingamizi 44 ya chaguzi kati hayo 13 yaliendelea na mengine yalienguliwa na kwa sasa kupitia uwezo wanaojengewa na shirika hilo wataweza kuyakabili mapingamizi mengi kwa haraka.Mkutano huo umefadhiliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la (UNDP), unalenga kutoa hamasa kwa majaji kushughulikia mapingamizi yanayojitokeza baada ya uchaguzi kwa kuzingatia misingi ya haki na kwa haraka ili kudumisha utawala wa sheria na demokrasia kwa upana wake.
Jaji kiongozi wa Mahakama Kuu nchini, Shaban Ally Lila amewataka watanzania kuondoa mawazo kuwa maamuzi yanayotolewa kwenye mahakama yanatokana na shinikizo la baadhi ya watu na badala yake wanatumia ushahidi na sheria katika kufanya maamuzi kwenye chombo hicho ambacho ni muhimili unaojitegemea
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Maswa, Talatius Kagenzi na Mwakilishi kutoka UNDP, Jaji Titus Osundina wamesema kuwa mafunzo hayo yatasaidia majaji na wasimamizi wa uchaguzi kuhakikisha kuwa uchaguzi unakua wa huru na wa haki
Tanzania inaelekea kwenye uchaguzi mkuu utakaofanyika 25 Oktoba mwaka huu ambapo taratibu mbalimbali za uchaguzi zinaendelea kufanyika ikiwemo uandikishwaji wa daftari la wapiga kura ili kutoa haki ya kidemokrasia kwa kila Mtanzania na kuhakikisha kuwa uchaguzi unakua wa huru na wa haki jukumu ambalo liko kwa vyombo husika, wanasiasa, serikali na kila Mwananchi.
0 comments:
Post a Comment