#Gazeti la Star: Wahalifu wasiachwe bila kuadhibiwa, asema Hollande
Rais wa Ufaransa, #Francois Hollande amempigia simu rais wa Uturuki
Recep Tayyip Erdoğan na kutoa rambirambi zake kufuatia shambulizi la
Suruç.
Rais Erdoğan alimueleza kuwa lengo la shambulio hilo ni
kuiondosha amani ya Uturuki, na mara moja watu waliohusika na tukio hilo
watakamatwa na kuwajibishwa.
Akiongeza kuwa Uturuki inapambana na
kundi lolote la kigaidi likiwemo DAESH, Erdogan alitoa wito kwa nchi
washiriki wa vita hii dhidi ya ugaidi kuonyesha ushirikiano wao.
#Gazeti la Haberturk: Awali rejareja, kisha faida kwa sekta ya magari
Makubaliano ya kuondosha vikwazo dhidi ya Iran yaliyotiwa saini na
nchi za Magharibi yataleta mabadiliko sana kwa uchumi wa Uturuki na ule
wa Umoja wa Falme za Kiarabu, UAE. Kwa mujibu wa ripoti iliyoandaliwa na
Merrill Lynch, Uturuki ni moja ya nchi 5 ambazo ni washirika wakubwa
wabiashara na Iran hasa katika sekta ya nishati na biashara za rejareja
na baadaye katika sekta ya magari.
Aidha kutokana na kuondoshwa kwa
vikwazo hivi, shirika la TUPRAŞ ambalo lilikua likinunua mafuta ghafi
kutoka Iran linategemewa kung'aa zaidi katika nyanja hizo.
#Gazeti lşa Yeni Şafak: Uturuki yaendelea kuvutia wawekezaji wa kigeni
Idadi ya wawekezaji wa kigeni imeendelea kuongezeka nchini Uturuki.
Uwekezaji wa kiasi cha dola milioni 846 ulifanywa kwa mwezi Mei na jumla
ya kiasi cha dola bilioni 4 milioni 905 katika kipindi cha miezi mitano
ya kwanza. Takriban mashirika ya kigeni 169 yalianzishwa mwezi Mei
mwaka huu huku makampuni 9 ya ndani ya nchi yakishirikiana katika
uwekezaji na mashirika ya kigeni. Nchi za Umoja wa Ulaya zinaongoza
katika orodha ya wawekezaji katika kipindi cha miezi 5 ya mwanzo.
Nchi
za Umoja wa Ulaya zzimewekeza kwa asilimia 44 ya uwekezaji wote, na nchi
za bara la Asia kwa asilimia 30.
#Gazeti la Milliyet: Wasanii wawili wa Kituruki mjini Beijing
Kazi za wasanii wawili wa Kituruki, Gonul Nuhoğlu na Elektra KB
zimechaguliwa na kıuingizwa katika makumbusho ya sanaa ya Yin Chuan
mjini Beijing.
Kazi ya Nuhoğlu inayojulikana kwa jina la "Castle" pamoja
na ile ya Elektra "Safari", "maandamano katika koloni la Wapalestina 2"
zimechaguliwa kuingia katika makumbusho hayo.
Home
MAGAZETI
Kama ilivyoada yetu, sasa ni muda wa kufanya uchambuzi wa vichwa vya habari vilivyopewa kipaumbele katika magazeti ya leo nchini Uturuki.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment