Kamishna wa Jeshi la Polisi mkoa wa Pwani, ACP Jafari Ibrahim akionesha
silaha zilizokamatwa na jeshi hilo katika mapori ya mkoa huo
Akizungumza na waandishi wa habari leo ofisini kwake Jafari Ibrahim, Kamishina Msaidizi wa Jeshi la Polisi (ACP) amesema, “…tulifanya opereshani na misako maeneo mbalimbali kati ya 20 Juni hadi 20 Julai mwaka huu. Tulifanikiwa kukamata bunduki aina ya SMG no. 14302621, risasi 30 za SMG ndani ya Magazine na visu 11.”
“Tulikamata bunduki mbili
zilizotengenezwa kienyeji, bunduki moja aina ya rifle, risasi 103 za
short gun, risasi 20 za SMG, jambia tatu, mapanga manne, bomu mlipuko wa
kutengeneza kienyeji matatu, vipande vidogo vya nondo 42, fyuzi
zilizotegwa 24, fyuzi zilizo tupu 56, water gel explosive tatu, silcon
rubber 100% na nyaya tatu za milipuko,” amesema ACP Ibrahim.
ACP Ibrahim amesema katika tukio la ukamataji silaha hizo pia wamefanikiwa kukamata watuhumiwa 27.
Aidha, amesema 12 julai mwaka huu katika
eneo la Misugusugu wilaya ya Kibaha walifanikiwa kumkamata Hassan
Justine maarufu kwa jina la Mbwambo (23) mkazi wa Kigogo Fesh jijini Dar
es Salaam, akiwa na silaha aina ya short gun yenye namba G.74533 wakati
akijiandaa kufanya uhalifu kwenye kituo cha mafuta cha Camel.
Justine amekiri kuhusika na matukio
mengine ya uporaji kwenye kituo cha mafuta cha Mogas eneo la Mwendapole
wilaya ya Kibaha na Mkata wilaya ya Handeni, Tanga.
“Tarehe 510 Mei mwaka hu, majira ya saa
nane usiku wilaya ya Kisarawe askari askari walifanikiwa kumkamata
mtuhumiwa Mohamed Kitumbi akiwa na vipande 24 vya meno ya tembo vyenye
uzito Kg 42 ndani ya mfuko wa sulphate akiwa amepakia kwenye pikipiki
yenye namba za usajili MC 660 AGP aina ya boxer vyenye thamani ya Sh.
182.7 milioni,” amesema ACP Ibrahimu.
Mbali na kukamatwa kwa vipande vya meno
ya tembo pia, 5 Julai walifanikiwa kuwakamata Jumbe Abdukarim Ngohengo
na Omary Yusuph wakiwa na noti bandia 370 za Sh. 10,000 wakiwa na lengo
la kuingiza fedha hizo kwenye simu za kupitia kwa wakala wa airtel
Money. Watuhumiwa wamefikishwa mahakamani.
ACP Ibrahim amesema, katika kipindi hicho
wamefanikiwa kukamata gunia 18 za bhangi zilizokuwa zinasafirishwa
kutoka Morogoro kwenda Dar es Salaam kwa gari namba T. 335 DCX, aina ya
Super Custom. Mtuhumiwa ni Maulid Abdalah, mkazi wa Manzese Midizini.
Mbali na kukamata bangi hiyo, pia
walikamata kilo 124 za mirungi zilizokuwa zikisafirishwa katika mabasi
yenye namba za usajili T. 678 CRT mali ya kampuni ya Burudan na gari
namba T.575 BLN mali ya kampuni ya Simba Mtoto.
Pia, walifanikiwa kukamata lita 88 za
pombe ya moshi, mitambo mitatu ya kutengeneza pombe hiyo na jumala ya
watuhumiwa 47 ambao ni watumiaji na wauzaji wa pombe hiyo walikamatwa na
kufikishwa mahakamani.
“Tunawaomba wananchi na wadau mbalimbali
kuendelea kuunga mkono juhudi zetu kwa kutoa taarifa za kiintelijensia
juu ya uhalifu ili mafanikio haya yaliyopatikana kwa kipindi cha mwezi
mmoja yawe na mafanikio endelevu na jamii iweze kuishi kwa amani na
utulivu,” amesisitiza ACP Ibrahim.
Source:http://mwanahalisionline.
0 comments:
Post a Comment