Image
Image

TIC kuwakusanya watanzania wa Ughaibuni.

SERIKALI nchini Tanzania kwa kushirikiana na Kituo cha Uwekezaji (TIC), cha Kimataifa kinatarajia kufanya kongamano la Diaspora jijini Dar es salaam.
Aidha, kongamano hilo litakalofanyika Julai 13 hadi 15 mwaka huu katika Hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam. Kongamano hili litakuwa la pili kufanyika hapa nchini na kuwashirikisha wadau mbalimbali.
Hayo yameelezwa leo jijini Dar es Salaam na Rosemary Jairo Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Diaspora kutoka Wizara ya Mambo ya Nje wakati alipokuwa akizungumza na waandishi.
Jairo amesema kuwa kongamano hili litatoa fursa kwa wafanya biashara wadogo kutangaza biashara zao kimataifa na kupata soko na mikoa nchini kutangaza fursa za uwekezaji zilizomo mikoani himo
Amesema kongamano la mwaka huu lina kauli mbiu Kuhamasisha Ushiriki wa Diaspora kukuza biashara ndogo na za kati nchini.
“kuwa kutakuwepo maonyeshoya biashara ,majadiliano ya mada kuhusu ushirikishwaji wa Diaspora katika maendeleo ya nchi hususani katika uwekezaji”amesema jairo
Amesema kuwa Kongamano hilo linatarajiwa kufunguliwa na Rais Jakaya Kikwete na kufungwa na Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Dk. Ally Mohamed Shein.
Aidha, Jairo amesema wadau wa kongamano hilo Diaspora ambao ni watanzania wanaoishi ughaibuni,wizara ya mambo ya Nje na Ushirikiano wa kimataifa, Ofisi ya Rais na Utawala Bora-zanzibar na Ofisi ya Waziri Mkuu
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment