Image
Image

Kenya yaapa kuchukuwa hatua kali dhidi ya silaha haramu zinazoingizwa nchini kinyume cha sheria.


Serikali ya Kenya imetangaza kwamba itachukuwa hatua kali na kutoa adhabu kwa wahusika wanaoingiza silaha haramu zinazochochea mizozo nchini.
Waziri wa Ulinzi wa Kenya Joseph Nkaissery pia aliarifu kuwa serikali itaongeza ulinzi na kuimarisha usalama kwenye mipaka ya nchi ili kuzuia uingizaji wa silaha haramu.
Silaha haramu zimekuwa zikitumiwa na makabila mbalimbali ya ufugaji yanayozozana na kwa visa vya wizi wa mifugo katika wilaya za kaskazini mwa Kenya.
Silaha hizo pia zinasemekana kutumika katika mashambulizi yanayotekelezwa na makundi ya kigaidi nchini Kenya.
Kwa mujibu wa takwimu za Wizara ya Ulinzi, takriban silaha 700,000 zinakadiriwa kumilikiwa na watu kinyume cha sheria nchini Kenya.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment