Image
Image

Rais Nyusi: ‘‘Mozambique inahitaji sheria mpya ili kuimarisha uwekezaji’’


Rais wa Mozambique Filipe Nyusi, alikutana na Rais wa Portugal Anibal Cavaco Silva katika ikulu ya Belem iliyoko mjini Lisbon.
Akizungumza na vyombo habari, Nyusi alisema kwamba Mozambique inahitaji sheria mpya ili kuweza kuimarisha sekta ya uwekezaji nchini.
Nyusi alifahamisha kwamba Portugal ni nchi ya nne kubwa inayowekeza zaidi nchini Mozambique na kwamba inahitaji kufunguliwa milango ili kuboresha sekta hiyo.
Nyusi aliongezea kusema kwamba serikali ya Mozambique inapaswa kuongozwa pamoja na sekta za kibinafsi ili kuweza kufikia maendeleo zaidi.
Portugal imekuwa nchi ya kwanza barani Ulaya kuweza kutembelewa na Nyusi tangu kuingia madarakani kama rais wa Mozambique.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment