Takriban wahamiaji haramu 2700 wameripotiwa kuokolewa katika pwani ya Libya walipokuwa wakijaribu kuvuka bahari kuelekea Ulaya.
Wahamiaji haramu hao wanaarifiwa kuokolewa na vikosi vya usalama vya Italia baada ya kusafiri masafa ya kilomita 55 kutoka kwenye pwani ya Libya.
Mizozo iliyozuka nchini Libya miaka minne iliyopita baada ya kiongozi wa nchi Muammar Gaddafi kuondolewa madarakani, imesababisha nchi hiyo kuzorota na kupelekea wananchi kutaka kutoroka.
Nchi ya Libya pia imekuwa kama njia kuu ya usafiri kwa wahamiaji haramu barani Afrika wanaotaka kukimbilia nchi za Ulaya.
Kwa mujibu wa takwimu za shirika la kimataifa la uhamiaji, takriban wahamiaji haramu 150,000 wanasemekana kuingia Ulaya hadi kufikia mwaka 2015.
0 comments:
Post a Comment