Image
Image

WATAFITI:Serikali iangalie upya bajeti iliyotengwa katika sekta ya kilimo.


Watafiti wa masuala ya bajeti wameishauri serikali kuangalia upya bajeti iliyotengwa katika sekta za kilimo na elimu ili kuwa ni kiwango sahihi cha bajeti iliyotengwa kutokana na thamani ya shilingi kuporomoka kwa kasi jambo ambalo ni dhahiri litaathiri bajeti ya sekta hizo muhimu na hivyo kutofikia malengo yaliyokusudiwa.

Watafiti hao wakizungumza jijini Dar es Salaam wamesema sekta ya kilimo bado ni muhimu katika kuwasaidia kiuchumi watanzania walio wengi hivyo ni vyema serikali ikaangalia upya bajeti hiyo kutokana na kuathiriwa na kupanda kwa dola jambo litakaloathiri utekelezaji wa miundo mbinu katika sekta ya kilimo na kuongeza usimamizi katika matumizi ya fedha hizo.

Kwa upande wake mtafiti na mhadhiri wa chuo kiku Jovita Katabalo amesema bajeti iliyotengwa licha ya kuonekana ni kubwa ikilinganishwa na sekta nyingine bado kuna changamoto nyingi ambazo bajeti hiyohaitaweza kuzitekeleza kutokana na bajeti ya maendeleo ya mwaka huu kuwa ni asilimia 27 tu huku sehemu kbwa ya fedha ikielekezwa katika matumizi ya kawaida ambayo hayawezi kusaidia kuendeleza elimu.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment