Wakati waisalamu dunia kote wakifanya maandalizi ya
kusherekea sikuku ya Eid el Fitr bei
za vitu mbalimbali hasa nguo za watoto na mahitaji mengine yenye
kuhusiana na sherehe hizo vimepanda bei
maradufu hatua ambayo imesasabisha baadhi ya watu kushindwa kununua mahitaji
yao katika maeneo maarufu ya biashara kariakoo jijini dar es salaam.
Tambarare
halisi imetembelea sehemu mbalimbali ikiwweo kariakoo na kusuhudia umati mkubwa
wawatu hasa wakina mama wakihaha kupata mahitaji yao huku wakilalamikia kupanda
kwa bei za vitu.
Baadhi ya wauzaji wa bidhaa hizo wamekiri kupanda
kwa bei za vitu ila na kusema kuwa
inatokana na kushuka kwa shlingi huku wengine wakisema kushuka kwa shilingi
kumekuja sambamba na msimu wa sikuu ndio
maana hali imekuwa mbaya zaidi.
Imekuwa
ni tabia ya wafanyabiashara na watu mbalimbali kupandisha bei za vitu kila
unapofika msimu wa sikuu za Eid
el Fitr kutokana na kuwepo kwa
mahitaji makubwa ya vitu hivyo huku
wakitoa sababu mbalimbali ambapo kwa
mwaka jana kisingizio kilikuwa ni kupanda kwa bei za mafuta lakini kwa mwaka
huu kisingizio wamedai ni kushuka kwa shilingi.
0 comments:
Post a Comment