Waziri wa ulinzi wa Uganda kuwasili nchini Burundi*Mazungumzo ya mzozo wa Burundi yaendelea.
Waziri wa ulinzi wa Uganda, Crispus Kiyonga aliwasili Julai 16 nchini Burundi kama ilivyofahamishwa na rais Museveni ili kuendesha mazungumzo ya amani yanayotarajiwa kukomesha mzozo wa kisiasa unaoikumba Burundi.
Mkutano ulifunguliwa ukiwa na umechelewa kwa muda wa masaa kadhaa.
Pande zote mbili, ikiwa serikali na upinzani waliwasili na kushiriki katika mkutano huo.
Kwa mujibu wa rais Museveni, serikali na upinzani nchini Burundi wana dhumuni moja moja ambalo ni kuweka umuhimu wa kuweka wazi namna ya kuendesha mazungumzo haraka iwezekanavyo.
Serikali ilileta utata baada ya kutoa tangazo linalotowa wito kwa raia kujihimiaza kupiga kura ifikapo Julai 21.
Jumuiya ya Afrika Mashariki ilipendekeza vipengele vitakavyjadiliwa ili kusuluhisha mzozo uliopo.
Mpatanishi alifahamisha kuwa vipengele vyote vitajadiliwa na kusema kuwa muhula wa 3, serikali ya muungano, kumiliki silaha kinyume na sheria, wafungwa wa kisiasa, bila kusahau suala ya vyombo vya habari ambavyo hadi sasa vimefungwa baada ya kuharibiwa vitajadiliwa.
AFP
0 comments:
Post a Comment