Wahalifu 10 wauawa na jeshi Burundi.
Watu 10 walikuwa na silaha wameripotiwa kuuawa baada ya kuvamia kambi ya jeshi Cibitoki, mkoa unaopatika kaskazini mwa Burundi.
Watu hao waliendesha shambulio dhidi ya vituo viwili vya jeshi usiku wa Ijumatano kuamkia Alkhamisi.
Jeshi la Burundi lilifahamisha kuwa lilifaulu kuwauwa wahalifu 10 waliokuwa wakijaribu kuyumbisha usalama mkoani humo ambapo kuna umbali wa kilomita 70 na jiji la Bujumbura.
Kamanda anaeongoza kambi ya jeshi ya Cibitoke, meja Ahishakiye Jean Baptiste aliliambia shirika la habari la aanadolu kuwa baada ya kuuawa kwa wahalifu hao, wengine watatu walijisalimisha.
Baadhi ya taarifa zinafahamisha kuwa huenda watu hao ni miongoni mwa wanajeshi walioasi na kuahidi kumuondoa kimabafu rais Pierre Nkurunziza kuwania muhula wa 3 katika uchaguzi wa rais mwaka 2015.
AA/Reuters
0 comments:
Post a Comment