Image
Image

Kura zaanza kuhesabiwa Burundi*Wawili wauawa hivi leo*Marekani yaukosoa uchaguzi huo.

Shughuli ya kuhesabu Kura imeanza nchini Burundi kufuatia uchaguzi wa urais ambao umeshutumiwa na wengi nchini humo na hata kimataifa.
Rais Pierre Nkurunzinza anatarajiwa kupata ushindi mkubwa kwa muhula wa tatu huku upinzani ukisusia kabisa kura hiyo.
Huku hayo yakijiri Marekani na Uingereza wamekashifu kura hiyo wakisema kuwa haikuwa ya huru na haki.
Marekani kwa upande wake imependekeza kugawana madaraka huku ikitishia kuchukua hatua dhidi ya Burundi iwapo muafaka hautapatikana.

  • Burundi:Uchaguzi wa urais.
Baada ya ghasia na maandamano ya miezi kadhaa, hatimaye jana raia nchini Burundi walifika katika vituo vya kupiga kura ili kumchagua rais wao.
Watu wawili wameuwawa usiku wa kuamkia leo katika mji mkuu Bujumbura.
                                          Uchaguzi wa urais umeanza Burundi
Mwaandishi wa BBC aliyeko nchini humo anasema kuwa, milio ya risasi na gruneti imesikika usiku kucha katika mji mkuu wa Burundi- Bujumbura.
Kiongozi wa sasa wa nchi hiyo anawania muhula wa 3 kama rais licha ya madai kuwa anakwenda kinyume na katiba ya nchi.
                          Foleni zimeonekana katika vituo vya kupigia kura
Viongozi wanne wa upande wa upinzani wameapa kususia uchaguzi huo.
Rais Pierre Nkurunziza, akiwaamevalia jezi ya michezo alipiga foleni katika kituo kilichokaribu na mji wa Ngozi alikozaliwa na kupiga kura.
                     Waangalizi wachache mno wanashiriki uchaguzi huu
Waangalizi wachache mno wanashiriki uchaguzi huu baada ya serikali ya Burundi kuwanyima vibali waangalizi wa Umoja wa Afrika katika muda wa lala salama.
Hata hivyo, waangalizi kutoka umoja wa Afrika Mashariki wapo huko kwa mwaliko wa rais Nkurunziza.
                   Viongozi wanne wa upinzani wamesusia uchaguzi huo.
Karatasi za kura zinaonesha kuwa kulikuwa na wagombea nane wa kiti cha urais lakini wanne kati yao wameshathibitisha kuwa hawatashiriki uchaguzi huo wakipinga hatua ya rais Nkurunziza kuwania muhula wa tatu.
Uchaguzi huu unafanyika licha ya taharuki kuhusiana na mgogoro wa kisiasa
Wagombea hao ni Agathon Rwasa, Jean Minani, Domitien Ndayizeye na Sylvestre Ntibantunganya.
                                           Wapiga wanamchagua rais Burundi
Jina la rais Nkurunziza na ishara ya chama chake imechapishwa miongoni mwa wagombea wa urais.
Saa chache tu kabla ya kufunguliwa shughuli ya upigaji kura, milipuko ya gruneti iliripotiwa jijini Bujumbura na kufuatiwa na milio ya risasi.
    Rais Nkurunziza ameonekana akipiga kura karibu na mji wa Ngozi
Katika maeneo mengine risasi zilisikika kwa wingi zaidi mjini humo. Japo haikuwa wazi ni nani hasa anayefyatua risasi hizo.
Viongozi wa upinzani wamesusia kushiriki uchaguzi huo kwa dai rais anakuka sheria kwa kuwania muhula wa tatu.
Kwa mujibu wa mshauri wa kisaisa wa rais, haya ni mashambulio yanayofanywa na 'magaidi' wanaonuia kuvuruga shughuli ya uchaguzi.
Hofu ya kuwa uchaguzi huu huenda ukalitumbukiza taifa hilo katika mzozo mbaya zaidi wa kisiasa imeifanya jamii ya kimataifa kuitisha kuahirishwa kwa uchaguzi na kupendekeza mashauriano ya amani.
Takriban watu 70 wamefariki katika maandamano ya awali kupinga uchaguzi huu.
Wito kama huu uliambulia patupu, mwishoni mwa wiki mashauriano ya amani yalivunjika na uchaguzi ndio huu unafanyika huku wito wa kuahirishwa kwake ukipuuziliwa mbali.
Takriban watu 70 wamefariki katika maandamano ya awali kupinga uchaguzi huu huku wengine zaidi ya elfu 160 wakiikimbia nchi kwa hofu ya kuzuka mapigano.

  • Marekani yazungumzia uchaguzi Burundi.
Marekani imesema uchaguzi wa Rais unaofanyika nchini Burundi umekosa uaminifu.
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nchi za nje wa Marekani John Kirby amesema zoezi hilo la uchaguzi lililogubikwa na utata ambao utaendelea kuipunguzia sifa serikali.
Pierre Nkurunzinza anawania awamu ya tatu madarakani, licha ya awamu mbili za kukaa madarakani zilizowekwa kwa mujibu wa katiba.
Wagombea wengi kupitia vyama vya upinzani wamesusia uchaguzi huo. Wakati huohuo katika kijiji cha Buye kaskazini mwa nchi, alikozaliwa Rais Nkurunziza mlolongo wa watu wamejitokeza kupiga kura.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment