Inafurahisha kuona kuwa wapo wafanyabiashara wengi maeneo tofauti tofauti
Nchini mwetu na mitaa tofauti tofauti wanaouza juisi ya miwa.
Kimsingi juisi hii ni sukari halisia ambayo haijachakatwa.
Sukari halisia ni nzuri kwa mwili kwani ina virutubisho na madini kwa
wingi.
Miwa ina faida nyingi kiafya.
Juisi ya miwa inafahamika na wataalamu wa afya kwa kuwa na uwezo wa kuupa
mwili nguvu kwa sababu ya ‘glucose’ iliyopo.
Kijiko kimoja cha juisi ya miwa,kina kalori 11. Madini halisi na vitamin
zinazopatikana katika sukari ni kama phosphorus, calcium, madini ya chuma na
potassium.
Si hivyo tu, miwa ni jamii ya tunda lenye alkali hivyo lina uwezo wa
kupambana na saratani hasa ile ya kibofu cha mkojo na saratani ya maziwa.
Miwa ina upekee wake kwani ina uwezo wa kuongeza maji mwilini, inaupooza
mwili na kuupa nguvu.
Virutubisho vilivyopo katika miwa vina manufaa makubwa katika kusaidia
utendaji kazi wa ogani muhimu kama figo,moyo, ubongo na viungo vya uzazi.
Pia, wagonjwa wa kisukari wasihofie sukari iliyopo kwenye miwa kwani
haina madhara yoyote kwao. Uzuri wa juisi ya miwa ni kuwa sukari yake ni
halisia.
0 comments:
Post a Comment