Imeripotiwa kwamba Messi alikua anatimiza ahadi yake ya kutembelea Gabon kwa Rais Ali Bongo ambae anashutuma nyingi za udicteta na kula rushwa. Bila kutegemea Messi akiwa na Deco walifika nchini Gabon na Messi kuweka jiwe la msingi kwenye ujenzi wa uwanja wa Taifa wa Gabon.
Ripoti zilizotoka kwa wana habari wa ufaransa zinasema kwamba Messi alipokea kiasi cha £2.4m ikiwa kama malipo yake ya kutembelea nchi hiyo. Mwanzoni ziara hiyo ilipewa picha kama ni ya kujitolea kwenda kuzindua uwanja wa taifa wa nchi hiyo.
Wachambuzi wa mambo wanasema kwamba kwa status ya Messi hata kama angepewa mualiko na Rais huyo ingekua sio rahisi kwa yeye kukubali kwasababu Rais huyo ana sifa mbaya ya kula rushwa. Pia ana kashfa ya kujilimbikizia mali wakati wananchi wake wana hali mbaya na nchi yake ina watoto wengi wanaoishi kwenye umaskini.
Wapinzani wa kisiasa wa Ali Bongo wanasema kwamba Rais huyo ametumia pesa za walipa kodi kumlipa Messi ambaye anajihusisha sana na mambo ya kujitolea duniani. Pia Ali Bongo inasemekana amemtumia Messi kwa ajili ya kujipatia ushawishi zaidi kwa wananchi wake.
Messi aliweka mikono yake kwenye cement mbichi ambapo mikono
yake itabaki kama kumbukumbu uwanjani hapo.Messi na Baba yake bado wana kesi ya
ukwepaji wa kodi nchini Hispania.
0 comments:
Post a Comment