Kwa kutumia akaunti ya twita Meek Mill ameandika
maneno yaliyomaanisha kwamba, Drake hawezi kuandika na mara nyingi amekuwa
akiandikiwa.
“Hata mimi niliwahi kumuandikia katika moja ya
albamu yake, lakini jamaa ameshindwa kuonyesha shukrani, ningejua nisingefanya
hivyo”, aliandika Meek Mill.
Meek Mill aliendelea kwa kusema kwamba marapa
wengi wanalijua hilo hata Lil Wayne na Nick Minaj ukiwauliza wataongea ukweli.
Naye Rick Ross alitoa maoni kwenye twita ya Meek
Mill na kuonyesha kukubaliana naye kwamba ni kweli Drake amekuwa akiandikiwa
nyimbo zake.
Pia Meek Mill aliwapongeza Kendrick Lamar na J.
Kole kwamba wawili hao wanajua sana kufanya muziki sema bado hawapo kwenye
laini nzuri.
Bado Drake hajajibu chochote kuhusu hilo, swalui
lilobaki je ni nini atakachokijibu baada ya tuhuma hizo toka kwa Meek Mill.
0 comments:
Post a Comment