Shahidi
huyo wa upande wa mashtaka alisema hayo jana mbele ya Hakimu Mfawidhi,
Cyprian Mkeha katika kesi inayomkabili Lipumba na wafuasi wake 30.
Akiongozwa
na Wakili wa Serikali Mkuu, Bernard Kongola alidai kuwa Januari 27,
mwaka huu, Kaimu Kamanda wa Polisi Temeke, Sebastian Zacharia alifika
karibu na Ofisi za CUF, Mtaa wa Boko Temeke, mkabala na Hospitali ya
Temeke na Benki ya NMB na kuelezwa hali ilivyokuwa.
Msuya alidai kuwa alimpa taarifa Lipumba kuhusu mkusanyiko wa watu uliokuwa na dalili za kuanzisha maandamano.
Alidai
kuwa ilipofika saa saba mchana, alimuona Lipumba na wanachama wake
wakiimba nyimbo zenye maudhui ya CUF, huku wakiwa na bendera na mabango
wakielekea yalipokuwapo magari ya polisi.
“Walipotufikia, Lipumba alishuka kwenye gari na kumuomba Kamanda Zacharia awaruhusu yeye pamoja na wafuasi wake kwenda Mbagala.
“Afande
Zacharia alimuuliza Lipumba kama alipata barua ya polisi ya kuzuia
maandamano na mkutano iliyoandikwa Januari 26, mwaka huu. Lipumba
alikiri kuiona, lakini akasisitiza yeye na wafuasi wake lazima waende
Mbagala.”
Aliendelea kudai kuwa Lipumba alishauriana na wafuasi wake na wao kama polisi walishauriana jinsi ya kuwazuia.
“Baada
ya kushauriana, tulibaini kuwa katika mazingira waliyokuwapo ya
hospitali na Benki ya NMB katika eneo hilo, tuliwacha wapite kwa vile
ingekuwa hatari kama tungeanza kuwazuia hapo.”
Alisema
baada ya muda, Lipumba na wafuasi wake na magari yao walipita
walipokuwapo askari kuelekea Mbagala, hivyo polisi wakaamua kupita njia
ya mkato ya Tandika Magengeni na kuwazuia katika eneo la Mtoni Mtongani.
“Tungepita barabara waliyopita wao tungeshindwa kuwazuia kwa sababu tungekuwa nyuma yao,” alisema.
Msuya
alidai kuwa wakiwa hapo, waliyaegesha magari yao barabarani na baadaye
Lipumba na wafuasi wake walifika na kuongea na Zacharia.
Alidai katika maongezi yao, Lipumba na wafuasi wake walitaka kuruhusiwa kwenda kwenye mkutano Mbagala Zakhem.
Alisema
walisogea katika mzunguko wa barabara katika eneo la Mtongani, lakini
bado wafuasi wa Lipumba walisisitiza kutaka kwenda Mbagala Zakhem.
Kamanda
Zacharia alimuagiza OCD Ramia Mganga kusoma ilani, ambayo wakati huo
ilikuwa imekwishanyooshwa mara tatu na kisha kurudiwa tena, huku
msisitizo ukiwa ni kuwataka kuondoka katika eneo hilo.
Aliwataka
waondoke vinginevyo ingetumika nguvu, lakini pamoja na amri hiyo,
wafuasi hao waliendelea kukaidi, ndipo nguvu ya dola ilipotumika.
Shahidi
huyo akihojiwa na Wakili wa Lipumba na wafuasi wake, Twaha Taslima
alidai kuwa Lipumba aliomba kwenda Mbagala kuahirisha mkutano. Kesi hiyo
imepangwa kuendelea kusikilizwa tena leo mahakamani hapo.
0 comments:
Post a Comment