Mnyika aliibua suala hilo jana bungeni,akitaka kusitishwa shughuli za Bunge ili suala hilo lijadiliwe kama jambo la dharula.
Alisema katika safari yake ya juzi kutoka jijini Dar es Salaam
kwenda Dodoma, alitembelea vituo vya mafuta zaidi ya nane na kukuta
huduma ya mafuta haitolewi kwa wateja.
Mnyika ambaye pia ni Waziri Kivuli wa Nishati na Madini, alisema
kauli ya serikali iliyotolewa bungeni kukanusha kuwapo mgomo wa wauza
mafuta si ya kweli.
"Kuna vituo vimegoma na vichache vimepandisha bei kupindukia, kwa
kuwa kuna waliyoyahodhi mafuta, shughuli za Bunge zisitishwe
tujadili,"alisema.
Hata hivyo, Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Charles Mwijage,
alisema jukumu la wizara ni kuhakikisha sekta hiyo inatulia kwa kuwapo
upatikanaji mafuta ambayo wananchi wanamudu na yenye viwango.
"Kuna ujumbe ulipitishwa juu ya uhaba wa mafuta, kabla ya taarifa
hizo tulishafanyia kazi kuhakikisha tuna mafuta ya hifadhi ya kutosha
siku 12 hadi 40,” alisema.
Alisema hivi sasa jitihada zinafanywa kwa kushirikisha Mamlaka ya
Mawasiliano Tanzania (Tcra) kuwatafuta waliosambaza ujumbe huo.
Mwijage alisema maofisa wa wizara yake walitembelea vituo nane na
kukuta hawauzi mafuta, lakini ilibainika kuwa ni kwa sababu hayakuwapo.
Alisema ikibainika kuwapo mfanyabiashara anayehifadhi mafuta pasipo
kuyauza, adhabu itakayomkabili ni faini ya Shilingi milioni 20 au
kufungiwa.
“Nimekuwa mkaguzi kwa zaidi ya miaka 30 hivyo naijua industry
(sekta) hii vizuri, Watanzania wawe na amani mafuta yapo aliyesambaza
ujumbe atakamatwa," alisema.
Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Fedha, Adam Malima, alisema kama kuna watu amehodhi mafuta, kuna sheria zinazowabana.
"Pale tulipo na uhakika wanafanya hujuma, serikali itachukua hatua
kali kwa aliye na mafuta, kuna vituo tumeenda hana mafuta, hii ni
serikali lazima ifanye kazi yake ipasavyo,” alisema.
Naye Naibu Spika, Job Ndugai, alisema anatambua lipo tatizo na
kwamba ifikapo kesho litakuwa limeisha hivyo haoni sababu ya kusitisha
shughuli za Bunge.
0 comments:
Post a Comment