Lowassa atarejesha fomu hiyo katika Ofisi za Makao Makuu ya CCM
Dodoma baada ya kukamilisha kazi ya kusaka wadhamini 450 kutoka mikoa
15 ikiwamo mitatu ya Zanzibar.
Mgombea huyo alihitimisha kazi ya kusaka wadhamini juzi mkoani Morogoro na jana alianza safari ya kuelekea Dodoma.
Akizungumza wakati akihitimisha safari yake ya matumaini Mkoani
Morogoro ya kusaka wadhamini, Lowassa alisema kuwa tayari ameshapata
wadhamini wa kutosha na wengine ataweka nyumbani kwake kama kumbukumbu.
"Nimezunguka mikoa yote 31 Tanzania bara na Visiwani, nimepata
wadhamini wengi hivyo nitapeleka idadi inayotakiwa 450 na haya mengine
yatakuwa kumbukumbu ya maisha yangu," alisema Lowassa.
Katika mikoa yote hiyo, Lowassa amepata wadhamini 874,297na alianza safari ya kutafuta wadhamini Juni 4, mwaka huu.
Katika ziara yake alikuwa akisisitiza wanachama kujiandikisha
katika daftari la kupiga kura ili wakati ukifika wapige kura bila
kupoteza haki yao ya msingi.
Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa na Katibu wa Halmashauri Kuu ya
Taifa Nec Idara ya Organaizesheni Muhammad Seif Khatib tarehe ya mwisho
ya kupokea fomu hizo ni kesho.
0 comments:
Post a Comment