Mkuu
wa shule hiyo yenye wanafunzi kuanzia shule ya awali hadi darasa la saba
Bi. Nazal Abraham anasema miundombinu ya shule hiyo ni chakavu kwa madai
kuwa shule hiyo ilijengwa tangu mwaka 1930 hadi sasa haijafanyiwa marekebisho
licha ya wanafunzi wanendelea kutumia madarasa hayo.
Amesema
walimu wanalazimika kutumia vyumba vitatu vyenye ufa ambavyo vimebaki
kufundishi wanafunzi hao kwa awamu hali inayosababisha elimu inayotolewa
kutokidhi viwango kutokana mazingira magumu ya kufundishia.
Kutokana
na tatizo hilo mamlaka ya elimu nchini (TEA )imetoa msaada wa shilingi milioni
30 pamoja na kuendesha harambee iliyofanikisha kupatikana kwa kiasi cha
zaidi ya shilingi milioni 83.5 kwa ajili ya ujenzi wa shule hiyo ambapo
mkurugenzi wa ukuzaji raslimali kutoka tea Bi. Silivia Lupembe anasema
mazingira wanayosomea wanafunzi ni hatari.
Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya
same Bw.Herman Kapufi ambaye aliongozana na wadau mbalimbali kutembea
shule hiyo amesema msaada wa haraka unahitajika huku baadhi ya wanafunzi
wakielezea changamoto zinazowakabili ikiwemo uhaba wa vyoo na walimu.
0 comments:
Post a Comment