Mwanasiasa Mkongwe na Spika wa Zamani wa Bunge la Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Pius Msekwa amesema kujitokeza kwa wingi kwa wagombea wa nafasi
ya Urais ndani ya Chama cha Mapinduzi ni kiashiria cha kukua kwa Demokrasia
ndani ya chama hicho.
Amesema kuwa licha ya muamko mzito na waaina yake lakini
bado ipo changamoto sasa yakuweza kuangalia ninani ambaye anaweza kuliongoza
taifa na kuwa mwenyekiti wa chama cha mapinduzi CCM.
Wingi huu wa watangaza nia sio mbaya ni mzuri tu lakini ikifika
wakati wakumsimamisha mgombea nashauri asije simamishwa mtu tu bali asimamishwe
mtu anaye kubalika si na chama peke yake bali anakubalika na wananchi kwa kua wao ndio
wenye maamuzi ya mwisho katika sanduku la kura na hapo ndipo uhai wa chama cha
CCM utakapo endelea kuimarika.
Akizungumza leo Asubuhi katika kipindi cha East Africa Breakfast, Msekwa
amesema kuwa suala hilo lilianza toka mwaka 1995 lakini wanachama walikuwa na
mwamko mdogo kujitokeza kuwania nafasi hiyo ila kwa kuwa sasa demokrasia
imepanuka ndiyo kumefanya wanachama wengi kujitokea wakati huu.Mh. Mswekwa amesema baada ya mfumo huo kuanzishwa mwaka 1995 na yeye alikuwa ni mmoja wa watu waliochukua fomu ambapo anasema alifanya hivyo baada ya kushawishiwa na wazee ndani ya chama hicho ili kuleta changamot ya wengine kujitokeza katika Kinyang'anyiro hicho.
Katika hatua nyingine amesema kwa sasa Chama cha Mapinduzi kimepoteza umaarufu wa kisiasa kutokana na wananchi kuonyesha dhidi ya serikali yao kutokana na kashfa mbalimbali kwa baadhi ya viongozi wake ikiwemo ya Epa na Richmond.
Amesema kuwa hali hiyo ya kushuka kwa chama ilijitokeza katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 baada ya mwaka 2005 kushinda kwa asilimia 80 lakini baada ya kashfa hizo ndio chuki kwa wananchi wakaweza kukifanya kushinda kwa asilimia 61.
0 comments:
Post a Comment