Image
Image

Wafungwa waasi na kupinga agizo la kuto vuta sigara Mjini Melbourne.


Mamia ya wafungwa kwenye  gereza lenye ulinzi mkali Mjini Melbourne nchini Australia  wameasi wakipinga agizo la kutovuta sigara ndani ya magereza linaloanza kesho.

Picha za televisheni zimewaonesha wafungwa hao wakiwa na fimbo ambazo wamezitumia kama silaha na wamefunik nyuso zao  katika gereza la  Ravenhall,lililopo  kwenye vitongoji  vy a  mji wa  Melbourne .

Shirika laUtangazaji la Australia  limesema wafungwa zaidi ya 300 wamehusika katika uasi huo.

Taarifa  zinasema nusu ya gereza hilo limefungwa na Polisi wa Australia wanajitahidi kurejesha hali ya utulivu kwenye gereza hilo.

Australia   imeshapiga marufuku uvutaji wa sigara kwenye maeneo ya hadhara kwa muongo mmoja uliopita, ikiwemo kwenye mighahawa,baa na maeneo ya kazi.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment