Image
Image

Mwanaume mmoja mkazi Chengdu nchini China anashikiliwa na polisi kwa kosa la kuchumbia hadharani.


Bwana mmoja mwenye umri wa miaka 27, Zhang Liang mkazi Chengdu nchini China anashikiliwa na polisi kwa kosa la kuchumbia hadharani.

Kwa mujibu wa mtandao wa Mail online, Zhang alikusanya watu zaidi ya mia moja katika eneo la Sichuan wengi wao wakiwa ndugu, jamaa na marafiki kwa lengo la kuomba ridhaa ya kumuoa mchumba wake wa muda mrefu zaidi.

Taarifa zinaendelea kueleza kuwa lengo la bwana huyo lilikamilika vizuri, kwa kuwa “bidada” alikubali lakini baada ya muda polisi walivamia eneo la tukio na kumkamata bwana harusi mtarajiwa.

Msemaji wa polisi mjini Sichuan, amedai kosa la Liang ni kutokutoa taarifa kituo cha polisi kuhusu tukio hilo aliloliandaa.



Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment