Image
Image

News Alert:Ajali yaua 10 baada ya basi la Simiyu Express kupasuka tairi Dodoma.

Watu kumi wamefariki dunia papo hapo na wengine 47 kujeruhiwa baada ya basi la kampuni ya Simiyu Express lililokuwa likitokea bariadi mkoani Simiyu kuelekea jijini Dar es Salaam kupasuka gurudumu la mbele ka kupoteza muelekeo na kisha kuparamia mti katika kijiji cha wilunze eneo la Chalinze nyama wilayani Chamwino Dodoma.
Kwa mujibu wa mashuhuda wamesema kabla ya ajali basi hilo lenye namba za usajili T318 ABM SCANIA lilikuwa kwenye mwendo mkali na wakasikia kishindo cha kupasuka Gurudumu na kupoteza muelekeo umbali wa zaidi ya mita 800 kisha kugonga mti wa mbuyu ambapo watu kumi walifariki dunia papo hapo huku idadi kubwa ya majeruhi ikiokolewa.

Akizungumzia chanzo cha ajali hiyo kaimu kamanda wa polisi mkoa wa Dodoma kamishina msaidizi David Mnyambugha amesema ni mwendo kasi ambapo mara baada ya gurudumu kupasuka  dereva alishindwa kulimiliki na ndipo likapoteza mwelekeo.

Kwa upande wake mganga mkuu wa mkoa wa dodoma Dk.Ezekiel Mpuya amethibitisha kupokea majeruhi 47 na miili 10 ya waliofariki dunia akiwemo dereva wa basi hilo aliyetambulika kwa jina la Salum Ramadhani shafi huku majeruhi waliolazwa kwenye hosipitali ya rufaa ya mkoa wa dodoma wakieleza namna ajali hiyo ilivyotokea.
Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa Dodoma Chiku Galawa ambaye pia ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa akizungumza katika eneo la ajali wamewataka wasafiri kutoa taarifa za mienendo mibovu ya madereva wawapo barabarani huku akitoa wito kwa wakazi wa dodoma na wasamaria wema kujitokeza kutoa misaada ya hali na mali kwa  majeruhi pamoja na kutambua miili ya marehemu.
Aidha ajali hiyo imesababisha kitengo cha damu salama mkoa wa Dodoma kuishiwa akiba ambapo mkuu wa kitengo hicho leah kitundya amewataka wakazi wa mkoa wa dodoma kujitokeza kuchangia damu kwani wapo baadhi ya majeruhi  wameshindwa kufanyiwa upasuaji kutokana na ukosefu wa damu.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment