Image
Image

Mkutano wa CHADEMA wavunjika mtwara*Wagombea watatu kati ya wanne wagomea uchaguzi.


Kura za maoni za kuchagua mgombea ubunge wa  jimbo la Mtwara Mjini na viti maalumu kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo-CHADEMA umevunjika baada ya wagombea watatu  kati ya wanne kugomea uchaguzi huo kwa madai uongozi wa wilaya umeshindwa kusimamia haki na hivyo kufanya kampeni katika kata 15 huku mgombea mmoja akifanya kampeni katika kata 17.

Hatua hiyo ikamlazimu msimamizi wa uchaguzi huo, CASTRO MONY ambaye ni Mwenyekiti kamati ya Umoja wa Katiba ya Wananchi-UKAWA Kanda ya Kusini  kuwahoji wagombea  watatu  na wajumbe ambao kwa kauli moja waliridhia uchaguzi huo uvunjwe.

Mkutano huo ulikuwa na wajumbe 160 wakiwamo makatibu kata, wenyeviti wa serikali za mitaa na matawi wameonesha kusikitishwa na tukio hilo,   na kutaka uongozi wa juu wa CHADEMA  kuwachukulia hatua viongozi chama hicho wilaya kwa kuvuruga uchaguzi huo.
Endelea kusoma taarifa zetu na Like ukurasa wetu hapo juu,Kwa Maoni ushauri tuandikie hapa.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment