Muimbaji nguli wa muziki wa Dance, Nguza
Viking maarufu kama Babu Seya pamoja na mwanae, Papii Kocha wameanza maandalizi
ya ujio wao mpya, ikiwa ni takriban miaka 14 tangu waachie kibao kipya.
Wawili hao walipewa msamaha na Rais Dkt John
Magufuli kwenye maadhimisho ya miaka 56 ya Uhuru. Serikali imeonesha nia ya
kuwasaidia waimbaji hao wanaopendwa sana kurejea tena kwenye muziki kwa
kishindo.
Naibu Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na
Michezo, Bi. Juliana Shonza aliwakutanisha na uongozi wa Wanene Studios
waliokubali kuchukua jukumu la kuwarudisha tena kwenye muziki.
Tayari wameanza kuingia studio kuandaa kazi
mpya katika studio hizo kubwa na bora zaidi katika ukanda wa Afrika Mashariki
na kati. Wameanza kwa kufanya photoshoot, kitu ambacho wamekiri kuwa ni kigeni
mno kwao kutokana na kuwa gerezani kwa miaka 14 na wametoka katika nyakati
ambazo muziki wa Tanzania umepiga hatua kubwa ukilinganisha na zamani.
“Miaka 14 si mchezo, mambo kama haya si
unayaona mwenyewe, niliyamiss, nimemiss vitu vingi, picha za ukweli, mambo haya
kule tulipotoka hamna. Lazima uelewe hii ni dunia nyingine,” alisema Papii
Kocha wakati wa photoshoot.
Kwa kujiamini, Papii amesema kuwa kazi zao
mpya zitakuwa kali zaidi ya zile za zamani. “Kwasababu tumejipanga vizuri na
kazi zinazokuja zitakuwa nzuri zaidi ya zile tulizofanya mwanzo,” amesisitiza
Papii. Kwenye photoshoot hiyo iliyofanywa na mpiga picha mahiri Eric Luga, Babu
Seya na Papii Kocha walivalishwa na mbunifu wa mavazi, Mtani Nyamakababi.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment