Viongozi wa shirikisho
la soka nchini TFF wametakiwa kuacha kuwabagua vijana wadogo wenye vipaji wanao
patikana katika mashindano mbali mbali yanayoendeshwa kwani kwa kufanya hivyo
kumekuwa kukikatisha tamaa kundi hilo na morali ya kufanya zaidi mazoezi.
Hayo yamebainishwa na
vijana kutoka taasisi ya kukuza vipaji ya Moro KIDS ya mkoani Morogoro wakati
wa mazoezi ya mchezo wa soka ambapo vijana hao wamesema kitendo cha TFF
kutowatumia vyema vijana kutoka taasisi mbali mbali za kuibua vipaji ikiwemo
kuwashirikisha kucheza katika timu ya taifa kumesababisha Tanzania kuendelea
kufanya vibaya kwenye mashindano mengi ya kimataifa huku kocha wa timu hiyo ya
vijana hussein mau akibainisha baadhi ya changamoto wanazokutana nazo.
Katika mchezo wa
masumbwi kocha mkongwe wa mchezo huo mkoa wa Morogoro, Pawa Iranda ametoa wito
kwa raisi atakayechaguliwa,sambamba na wadau wengine wa mchezo huo kuupa sàpoti
mchezo wa ngumi ikiwemo kusaidia mahitaji mbali mbali kama udhamini na vifaa
ili kuweza kuufikisha mbali mchezo na kuitangaza nchi kimataifa kama alivyoweza
kuipeperusha vyema bendera ya tanzania ndani na nje ya nchi bondia wa
ngumi za kulipwa Francis Cheka na mabondia wengine.
0 comments:
Post a Comment