Moja kati ya sababu zinazotajwa kuchangia wanafunzi wa shule za msingi na sekondari katika wilaya ya uyui mkoani Tabora kushindwa kujua kusoma na kuandika inatokana na kutokuwepo kwa vitabu vya masomo mbalimbali vikiwemo vya ziada na kiada,hatua ambayo pia imewaondolea moyo wa kujisomea kwa wanafunzi wanaojua kusoma.
Akizungumza kwa niaba ya Afisa Elimu wilaya ya Uyui wakati wa hafla fupi ya kukabidhi Msaada wa vitabu vilivyotolewa na Mradi wa vijiji vya Milenia Mbola,Afisa Elimu Vielelezo Bw.Cassian Luoga,amesema bado kumekuwa na tatizo la upungufu wa vitabu katika shule za msingi na Sekondari Wilayani Uyui na hivyo kukwamisha kasi ya maendeleo ya Sekta ya Elimu mashuleni.
Aidha Bw.Luoga pamoja na kutoa shukrani kwa Mradi wa vijiji vya Milenia mbola kwa kutoa msaada huo wa vitabu hivyo vyenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 23,amewataka Wazazi wa wanafunzi kujenga tabia ya kushirikiana na Serikali kuchangia maendeleo katika sekta ya elimu,huku Mratibu wa Elimu wa Mradi wa vijiji vya Milenia Mbola Bw.Nemes Temba akitaja malengo mahususi ya msaada huo katika kuinua kiwango cha elimu kwa wanafunzi.
Kwaupande wake Mwalimu mkuu wa moja kati ya Shule nne zilizopata msaada huo wa vitabu,Shule ya Msingi Madaha Bi.Catherine Mmbando amesema msaada huo umekuja wakati muafaka ambapo Shule hizo hazina vitabu vya kutosha kukidhi mahitaji ya kufundishia
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment