Image
Image

Uturuki kupambana dhidi Daesh na PKK.


Rais Recep Tayip Erdogan amefahamisha kuwa Uturuki inapambana dhidi ya wanamgambo wa Daesh na wale wa PKK.
Rais Erdogan alifahamisha kuwa maeneo yanayounga mkono na kusapoti ugaidi yamesalia kimya bila ya kulaani shambulio lililopelekea watu 32 kuuawa Sanliurfa.
Rais Erdogan alisema kuwa kitenda cha kusalia kimya ni aibu kubwa kwa ulimwengu unaodai kupambana dhidi ya ugaidi.
Erdogan alilaani vikali shambulio lililopelekea kuuawa kwa askari polisi wawili Ceylanpinar ambalo kundi la kigaidi la PKK lilijinasibu kuendesha shambulio hilo.
Rais Erdogan alilaani vikali pia shambulio la Suruc ambapo watu 32 waliuawa Sanliurfa.
Rais Erdogan alizidi kufahamisha kuwa Uturuki itafanya kila liwezekanalo ili kuwakamata na kuwafikisha mbele ya vyombo vya sheria waliohusika na mashambulizi hayo.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment