Wizara ya Afya ya Kenya imeondoa agizo la ulazima wa nchi nzima kuvaa barakoa ikiwa ni mwongozo uliorekebishwa na kutolewa hii leo.
Katika agizo hilo jipya, Kagwe amesema karantini ya
lazima, na kutengwa kwa kesi zilizothibitishwa za Covid-19 kumesimamishwa mara
moja, na kuongeza kuwa wagonjwa wasio na dalili pia hawatahitaji kutengwa.
Aidha, ukomo wa idadi ya watu katika maeneo ya
kuabudu kwa wale waliopata chanjo pia imeondolewa, Waziri wa afya nchini Kenya
Mutahi Kagwe amesema.
Uchunguzi wa joto la lazima na uvaaji wa barakoa
katika maeneo ya wazi na ya umma pia umeondolewa, isipokuwa kwa mikusanyiko ya
ndani.
Hatua hii inafuatia kupungua kwa kiwango cha
maambukizi ya Covid-19 na visa vikali nchini.
Wakati wa mkutano na waandishi wa habari uliofanyika
leo, Waziri wa Afya Mutahi Kagwe amesema viwango vya kuthibitisha kuwa na
Covid-19 vimesalia chini ya 5% kwa mwezi mmoja uliopita.
Hata hivyo waziri huyo wa afya amehamasisha umuhimu
wa kuvaa barakoa na kuendeleza hatua ya kutokaribiana. Pia amesema kuwa hatua
ya kuwekwa karantini itasitishwa.
0 comments:
Post a Comment