Image
Image

Norway imeipatia Tanzania shilingi milioni 6.9 kusaidia kuwahudumia wakimbizi wanaoingia nchini.


Serikali ya Norway imeipatia Tanzania shilingi milioni 6.9 kwa ajili ya kusaidia kuwahudumia wakimbizi wanaoingia nchini.
Makubaliano ya ruzuku hiyo yamesainiwa jijini Dar es salaam kati ya balozi wa Norway hapa nchini Mheshimiwa HANNE MARIE KAARSTAD  na Mrakibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Tanzania Bwana ALVARO RODRIGUEZ.
Taarifa ya ubalozi wa Norway jijini Dar es salaam imesema fedha hizo zitasaidia shughuli za serikali katika kuwahudumia wakimbizi.
Balozi wa Norway nchini Tanzania Mheshimiwa  HANNE-MARIE KAARSTAD  amesema Tanzania imeonesha mfano mzuri  wa ushirikiano kati yake na mashirika ya Umoja wa Mataifa.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment