Obama aendeleza mazungumzo yake na viongozi wa jumuiya ya kimataifa baada ya mkataba wa Iran.
Rais wa Marekani Barack Obama, amefanya mazungumzo na Rais wa Urusi Vladimir Putin kwa njia ya simu.
Baada ya mahusiano kati ya Marekani na Urusi kufifia kufuatia mzozo wa Ukrein, kumekuwa na mwamko mpya kati ya nchi hizo mbili kutokana na mkataba wa nyuklia wa Iran.
Obama alimpongeza Putin kwa mchango wake katika mchakato wa maelewano kuhusu mkataba wa nyuklia wa Iran uliodumu kwa kipindi cha miezi 20.
Katika mazungumzo yao, viongozi hao wawili walidhihirisha ushirikiano wao kwa lengo la kutaka kumaliza mizozo ya katika kanda.
Hata hivyo, suala la Ukrein halikujadiliwa kwenye mazungumzo hayo kati ya Obama na Putin.
0 comments:
Post a Comment