Faida za tunda la parachichi au avocado.
Tunda hili ni lenye faida nyingi kiasi kwamba baadhi ya watu wamelipa
jina la malkia wa matunda.
Kuna ambao wamethubutu kuliita parachini
kuwa ni aina nyingine ya ndizi na ingawa huko nyuma tunda hilo
halikuzingatiwa sana lakini kutokana na faida zake nyingi kiafya na pia
katika masuala ya vipodozi, hivi sasa avocado ni miongoni mwa matunda
yanayosifika sana duniani.
Tunda hili lina kiasi kidogo cha maji tofauti
na matunda mengi tuliyozea kula,lina kiwango kikubwa cha mafuta na
ndani yake pia kuna tindikali (ACID) aina mbalimbali zinazosaidia
kukinga na kutibu maradhi mwilini.
Parachichi pia lina kiwango cha juu
cha protini na pia vitamin E.
Inaelezwa kuwa,vitamin E iliyoko wenye
avocado ni nyingi zaidi kuliko ile inayopatikana kwenye vyanzo vya
wanyama,na kwamba hata mayai hayana kiwango kikubwa cha Protein
ikilinganishwa na avocado.
Sifa hiyo inalifana parachichi kuwa tunda
linalopendwa sana kuliwa na wanamichezo hasa wale wanaopenda kujenga
miili yao kwa kutumia amino acids.
Virutubisho vingine vinavyopatikana
kwenye avocado ni vitamin B6,madini ya chuma na madini ya potassium.
Tunda la avocado ni chakula kizuri kwa watoto hasa kutokana na ulaini
wake,na virutubisho lilivyonavyo vinaweza kuwapa nafuu wale wenye
matatizo ya mfadhaiko na matatizo ya uzazi kama ugumba na utasa.
Tindikali aina ya oleic iliyomo ndani ya parachichi inasaidia kukinga
magonjwa ya moyo, kiharusi na kansa.
Aidha tunda hili linasaidia
uyeyushaji wa chakula tumboni hasa kwa wale wenye matatizo ya vidonda
tumbo,kwani lina ufumwele ambao ni muhimu katika kukinga kuta za
utumbo. Wale wenye kusumbuliwa na ukosefu wa damu,kisukari,matatizo ya
mfumo wa neva na mishipa ya damu wanashauriwa kula avocado mara kwa
mara.
Pia tunda hili limethibitishwa kupunguza kiwango kikubwa cha
mafuta mabaya ya cholesterol kwenye damu hasa kwa watu ambao ni wanene.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment