Tunda la embe
umbo lake hutofautiana,mengi yao
huwa aidha na rangi ya kijani, manjano ama nyekundu. Embe inaweza kuiva ikiwa
mtini lakini ili kuzuia uharibifu kutoka kwa ndege na popo ambao hula tunda
hili, wakulima huamua huvuna mara tu inapokomaa kwa kuangusha ikiwa bado
haijaiva.
Utagundua
kuwa embe imekomaa kwa kuiangalia rangi kwani hubadilika kutoka rangi ya kijani
hadi ya manjano au nyekundu. Kuna aina nyingi za embe kama vile embe dodo, embe
mali, embe bolibo, embe nuka, embe kidney, embe Julie Manzano na kadhalika.
Watu wengi
hupenda kula embe ikiwa imeiva lakini ulaji wake ikiwa bado mbichi ni jambo
muhimu sana kiafya. Nyama ya tunda hili ni tamu pia ina virutubisho kwani ni
chanzo cha upatikanaji wa vitamini A na C mwilini mwa binadamu.
Embe ina
kiasi cha wastani cha thiamin na niacin na asilimia 10 hadi 20 ya sukari
inayosaidia mwili iwapo mtu anakula tunda hili. Maembe pia yanaweza
kugandishwa, kukaushwa kwa jua na kuweza kutumika siku nyingi
zijazo. Maembe pia yanaweza kuwekwa kwenye makopo viwandani ama kupikwa
katika jemu na watu kutumia baada ya muda fulani.
Lakini embe
pia hutumika kutengeneza jeli, pai, achari kama Mengo pickle ambayo hupendwa na
watu wengi na kwa hakika huwa ghali kutokana na tunda lenyewe kupendwa na watu.
Kuna watengenezaji wa aiskrimu huamua kutumia tunda hili kutengeneza na wengi
hupenda kutumia kutokana na harufu yake nzuri.
Watu wengi
hutumia tunda hili kutengeneza juisi ama ikiwa yenyewe tu au kwa kuchanganya na
matunda mengine. Matunda ambayo hutumika kuchanganya na embe ni ndizi, nanasi,
parachichi, zabibu, papai na kadhalika.
Kuna wengine
hutumia mchanganyiko huo kwa kula bila kusagwa na wengine huamua kusaga na
kugeuza kuwa juisi ambayo inaweza kutumika bila kuongeza sukari kwa kuwa
matunda hayo yote yana sukari ndani yake.
0 comments:
Post a Comment