Nguli wa soka wa Brazil Rivaldo (43)
usiku wa jana aliingia katika headlines za soka baada ya kucheza mechi na mtoto
wake Rivaldinho na wote
kufunga magoli katika mechi moja.
Headlines hapo mtu wangu sio tu
kufunga wote katika soka ila ni Rivaldo kurejea
tena uwanjani na kuifungia bao timu hiyo baada ya kutangaza kuustafu 2014
lakini hivi karibuni alirejea tena uwanjani na klabu yake ya Mogi Mirim iliomlea toka 1992-1994 ambayo pia kwa
sasa yeye ni raisi wa klabu hiyo.
Rivaldo ambaye alifunga bao la pili kwa mkwaju wa penati baada ya
mwanayeRivaldinho kufunga bao la kwanza kwa kichwa na baadae kufunga la
tatu na kuipa ushindi timu yao wa magoli 3-1 dhidi ya Macae, yaani
mtu wangu ni mchezo ambao ulitawaliwa na baba na mwana tu.
Rivaldo alimzaa Rivaldinho 1995
akiwa na umri wa miaka 23 wakati huo ambao alikuwa anaitumikia klabu ya Palmeiras ya Brazil.
Mtu wangu nimekuwekea video ya
magoli waliofunga Rivaldo na mwanaye hapo chini.
0 comments:
Post a Comment