Rais KIKWETE ambaye aliondoka nchini Jumamosi Usiku kwenda nchini
AUSTRALIA anafanya ziara hiyo rasmi ya Kiserikali katika Jumuiya ya
Madola ya AUSTRALIA - The Commonwealth of Australia kwa mwaliko wa
GavanaJenerali Mstaafu wa Jumuiya ya Madola ya AUSTRALIA Sir PETER
COSGROVE.
Wakati wa ziara yake, Rais KIKWETE ambaye mara ya mwisho alitembelea
AUSTRALIA kuhudhuria MkutanowaWakuu wa Serikali wa Nchi za Jumuiya ya
Madola Mjini PERTH mwaka 2011, atatembelea Mji Mkuu wa AUSTRALIA wa
CANBERRA na miji ya NEWCASTLE na SYDNEY.
Katika ziara yake nchini humo hii Leo Rais KIKWETE atapandaMti wa
Kumbukumbu katika Bustani yaTaifa yaMiti ya AUSTRALIA na kutembelea
Makumbusho yaTaifa ya Vita ya nchi hiyo kabla ya kukutana na Watanzania
wanaoishi nchini AUSTRALIA.
Siku ya Jumanne Rais Kikwete atafanya mazungumzo rasmi ya Kiserikali
na Waziri Mkuu wa AUSTRALIA, TONY ABBOT ambapo pia atakutana kwa
mazungumzo na mwenyeji wake Gavana Jenerali Sir PETER COSGROVE ambaye
alipata kuwa Mkuu wa Majeshi ya AUSTRALIA.
Jumatano, Rais Kikwete atakwenda mjini NEWCASTLE ambako atatunukiwa
Digriii ya Uzamivu yaHeshima yaSheria na Chuo Kikuu cha NEWCASTLE.
Rais atatunukiwa digrii hiyo ya heshima kwa kutambua uongozi wake
uliotukuka na mchango wake katika maendeleo ya TANZANIA na AFRIKA na
jitihada zake za kuleta amani.
Rais KIKWETE na ujumbe wake wataondoka AUSTRALIA aAlhamisi, Julai 30 kurejeanyumbani.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment