Image
Image

Rais JAKAYA KIKWETE amewataka watendaji wa wizara ya Maendeleo ya mifugo na uvuvi kubadilika kifikra.

Rais JAKAYA KIKWETE amewataka watendaji wa wizara ya Maendeleo ya mifugo na uvuvi kubadilika kifikra na kuongoza mapinduzi ya ufugaji wa kisasa nchini ili kuongeza tija katika mazao yatokanayo na mifugo hatimaye yachangie kikamilifu ukuaji wa pato la taifa kutoka asilimia 4 za sasa.
Akizungumza katika uzinduzi wa mpango wa kuboresha na kuendeleza sekta ya mifugo nchini,Rais KIKWETE amewataka watendaji wa wizara hiyo kuharakisha matumizi ya teknolojia ya ufugaji na kuongeza mnyororo wa thamani kwa kupata mbegu bora za wanyama,vyakula vya mifugo, viwanda kwaajili ya uvunaji bora wa mazao yatokanayo na wanyama pamoja usafi wa bidhaa hizo.
Rais JAKAYA KIKWETE amezindua mpango wa kuboresha na kuendeleza sekta ya mifugo nchini ambapo jumla ya dola bilioni 1.7 zitatumika katika mpango huo utakaowashirikisha wafugaji wadogo na wakati.
Akizungumza mara baada ya uzinduzi wa mpango huo, rais KIKWETE amesema TANZANIA imebarikiwa kwa kuwa na mifugo mingi baada ya SUDAN KUSINI na ETHIOPIA ambapo asilimia 37 ya Watanzania wanategemea mifugo,lakini mchango wa mazao ya mifugo katika pato la taifa haurizishi.
 Hata hivyo jitahada za kufikisha elimu na uelewa juu ya umuhimu wa matumizi ya teknolojia ya ufugaji wa kisasa kwa walengwa ni changamoto inayohitaji kufanyiwa kazi.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment